The Chant of Savant

Sunday 30 July 2017

Waswahili Wasiojua Mateso na Umaskini wa Magabacholi Watazame Video Ifuatayo


Kwanini Hamad na Lipumba wamejivika kitanzi?

Image result for photos of lipumba and hamad
 
            Bila shaka wapenda demokrasia na mabadiliko nchini watakuwa wanasononeshwa, kushangazwa hata kuchoshwa na mgogoro usio na tija kwa taifa kwenye Chama Cha Wananchi (CUF) ambapo mwenyekiti wake Profesa Ibrahim Lipumba na Katibu mkuu Seif Sharrif Hamad wamo kwenye mbio za kukiua chama; sijui wapate nini na kwanini na faida ya nani zaidi ya uroho wa madaraka; na kutoweza kuona mbali. Siamini kama Hamad na Lipumba hawajui wanachofanya pamoja na madhara yake ya muda mfupi na muda mrefu. Sijui kama kuna mshindi katika mtanziko huu wenye kila ishara za kuua chama na kudhoofisha upinzani kwa ujumla. Je wawili hawa wanatumika au wameamua kujitumia ili watesi wao waendelee kupeta kama wasemavyo watoto wa mjini?  Hii si mara ya kwanza wala ya mwisho kuwashauri wawili hawa kuwa wanachofanya hakiendani na dhana nzima ya upinzani na demokrasia ya vyama vingi. Sijui kama wanaangalia walikotoka ili wajue waendako au wanakwenda waendako kinyumenyume wasijue wanarudi nyuma.        Je Hamad na Lipumba watapata faida gani zaidi ya kugeuzwa vikaragosi kisiasa kiasi cha kutumika kama wenzao walioua vyama au kushindwa kuvikuza? Kwanini hawajifunzi toka kwa Augustine Mrema na yaliyompata baada ya kuua vyama kadhaa akaishia kuwa kiraka kisiasa? Je katika mkasa huu wa kujitakia nani wa kulaumiwa baina ya wawili hawa? Tuwalaumu wote au mmojawapo? Je wawili hawa wameweka maanani maslahi mapana na ya muda mrefu ya wananachama wa CUF? Je ugomvi wa wawili hawa unafichua kile kilichofichwa muda mrefu kuwa wanatumiana bila kujua au kwa kujua kila mtu akingojea zamu yake kama ilivyotokea kwa Lipumba baada ya kumfukuza Hamad na baadaye wabunge wote waliokuwa wakimuunga mkono? Je kinachoendelea ni ushahidi kuwa wawili hawa wameishi kwenye ndoa ya mashaka ukiachia mbali kuwa kwao cha muhimu ni madaraka kuliko maslahi mapana ya wananchama? Je kinachoendelea ni ushahidi kuwa chama hiki ni mali ya watu binafsi tena wawili lakini si wanachama?
            Kwa wanaojua historia ya CUF na kilichompata mwanzilishi wake, James Mapalala ambaye kimsingi kilimpata sawa na kilichompata Hamad ambaye alimpoka chama, hawashangai kinachompata Hamad kwa sasa. Ukiishi kwa upanga, utakufa kwa upanga. Ukidhulumu utadhulumiwa na ukipiga utapigwa. Kawaida, unavuna ulichopanda.
            Wanaojua namna Hamad alivyokuwa akikigeuza chama kama akaangaye samaki, wapo waliokuwa wakishangaa na kutoshangaa kilichompata hatimaye. Maana wakati akiwa ndiye kila kitu kwenye chama enzi zile, wengi walikuwa wakihoji; inakuwaje mtu mwenye shahada moja amtumie profesa wasijue kuwa naye aliyeonekana kutumiwa alikuwa akipiga mahesabu yake akimtumia aliyedhaniwa kumtumiwa kwa namna yake. Ni bahati mbaya sana. Hamad alidhani atamtumia Lipumba atakavyo kufikia malengo yake binafsi asijue na mwenzie alikuwa naye akipiga mahesabu yake. Ni sawa na kale ka mchezo ka Magomeni ambapo matapeli wawili walifanya biashara huku mmoja akimuuzia mwenzie cheni feki asijue amelipwa fedha feki. Ngoma droo. Kwanini dhana hii? Hamad, siku zote, aliekeza nguvu zake Visiwani huku akimweka Lipumba kama kikaragosi cha kuaminisha Bara kuwa Hamad alilenga kufanya siasa za Muungano. Rejea alivyoamua kuingia serikali ya Umoja wa Kitaifa (GNU) Visiwani bila kutaka irudufiwe Bara. Rejea kulalamikia kuibiwa urais Visiwani lakini si Bara. Hamad anapaswa aambiwe. Janja yake haitamfikisha mbali. Pia Lipumba aelezwe, wanaomshabikia na kumtumia kwa sasa, wakishamalizana naye watamtupa kama ganda la muwa la jana. Kwa vile wawili hawa wameweka historia (precedent) mbaya, sitashangaa siku moja Lipumba, kadhalika, akanyang’anywa chama kama alivyomfanyia Hamad sawa naye alivyomfanyia Mapalala.
            Wawili hawa wanapaswa kufahamu kuwa chama si kama mpira wa kunyang’anya kufikia kufunga magoli. Chama ni tofauti kabisa. Ni rahisi kukibomoa na vigumu kukijenga. Hili liko wazi; na naamini wawili hawa wanalijua. Sema wanajifanya kutoliona au wanapofushwa ima na uroho wa madaraka au mipango binafsi fichi.
             Kitu kingine wanachopaswa kufanya wawili hawa ni kuonyesha njia na kuwa sehemu ya suluhu ya matatizo yanayoikabili CUF ambayo, kimsingi, walianzisha wenyewe. Wasiendelee kujiruhusu kuendelea kuwa tatizo badala ya jibu la matatizo ya chama. Niliwahi kushauri kuwa wanachama wa CUF warejeshe chama chao mikononi mwao kwa kuhakikisha wanawafukuza wawili hawa ili kuendeleza yale waliyodhamiria kwenye kuanzisha na kujiunga na chama hiki kikiongwe nchini. Kama kweli Lipumba na Hamad wako serious na siasa za upinzani zinazolenga kuikomboa Tanzania nzima, wanapaswa kukaa kitako kwenye meza ya duara na kuzika tofauti zao kama njia mujarabu ya kutatua matatizo yanaoendelea kukidhoofisha na hatimaye kukiua chama. Kama haiwezekani basi mmoja akubali kushindwa aanzishe chama kingine kuliko kung’ang’ania chama kimoja mnachozidi kukidhoofisha.
            Tumalizie kwa kuwaasa Hamad na Lipumba kuwa wakiendelea na mchezo huu walioanzisha, watakuwa sawa wanaojivisha kitanzi. Mwishowe, watakufa wote. Hakuna atakayejeruhika; kwa vile hakuna wa kukata kitanzi walichojivisha kabla ya kuwaua kikatili. Hata hivyo, Hamad na Lipumba wanao uwezo wa kuchagua kifo kisiasa badala ya kusuluhisha tofauti zao na kusonga mbele.
Chanzo: Tanzania Daima J'pili leo.

Friday 28 July 2017

Kafulila, Magufuli,Tumbili na We-rema

Farewell Robert Mugabe!

Image result for photos of robert mugabe dosing
For over a month, I have been grappling with this awkward idea. I must admit. I don’t hate Robert Mugabe. However, my crystal ball tells me that he is in the beginning of his end in power and on earth. I don’t know why this idea has stuck with me. It is my first time to have written about the exit of a person. Some would think; I am a doomsayer. I am not even a priest like the one who predicted the death of Mugabe. Nay; I am not; and I don't intend or wish to be. Again, this is the idea that is tormenting my head. I can see the new beginning for Zimbabwe. I therefore would like to share my premonition with my readers. How long will it take for Mugabe to come to an end? I truly don’t know. However, I still feel that his days are now numbered. Am I right or wrong to write this? Time will tell.


Wednesday 26 July 2017

Time for our neighbours to right their past mistakes

Baada ya Escrow Lugumi na UDA nao watumbuliwe


                        Hivi karibuni rais John Magufuli aliwafurahisha watanzania kiasi cha kuwaaminisha kuwa ufisadi hauna nafasi katika nchi yetu. Ni baada ya kuchukua hatua za makusudi na za kupongezwa za kuwakamata na kuwafikisha mahakamani watuhumiwa wa kashfa ya wizi wa mabilioni ya fedha toka kwenye fuko la Escrow. Kimsingi, hatua hii adimu na adhimu ilizidi kuongeza imani ya umma kuwa kumbe hakuna asiyeguswa japo bado wapo marais wastaafu ambao serikali zao ziliingiza kampuni la Independent Tanzania Power Limeted (IPTL) ambalo ndiyo mama wa wizi na uhujumu huu.
            Tokana kuanza kuishughulikia kashfa ya Escow kisheria, wengi wanaamini mwisho wa yote mkono mrefu wa sheria utatua IPTL. Pamoja na hatua hii ya kutia moyo, wengi wangetaka rais Magufuli aende mbali na kuwakamata watuhumiwa wengine ambao walihujumu taifa na kuliingiza hasara ya mabilioni ya shilingi. Leo, bila kuficha wala kumung’unya, tunamkumbusha rais Magufuli kuwa bado kuna kashfa nyingine kama vile Lugumi ambapo kampuni iitwayo Lugumi Enterprises Limited inadaiwa kupewa tenda na jeshi hilo kwa ajili ya kufunga mashine za kuchukua alama za vidole – ‘Biometric Access’ katika vituo 108 nchi nzima kwa gharama ya Sh bilioni 37. Mpaka kashfa yenyewe inaibuka Lugumi iikuwa imefunga mashine katika vituo 14 pekee wakati ilikuwa tayari imeishalipwa Shingili bilioni 34 ambazo ni sawa na asilimia 99 ya fedha zote za mkataba. Kuna haja ya kuchunguza mazingira na sababu za kufanyika kwa malipo haya kwa kampuni ambayo ilikuwa haijafanya kazi yoyote ukiachia mbali kuchunguza historia ya kampuni ya Lugumi na wamilki wake.
            Je, kama hakukuwa na namna, ilikuwaje kampuni hiyo ikapewa malipo ya asilimia 99 bila kuwa imetekeleza angalau asilimia sawa za kazi iliyokuwa iifanye? Maana, kiakili na kisheria ni jambo lisilowezekana bila kuwa na namna yoyote haramu ya kupinda au kuvunja sheria. Je Lugumi ni kikaragosi kilichotumiwa na wakubwa fulani kuliibia taifa?
            Kuna taarifa ambazo hazijawahi kupingwa kuwa Lugumi ni mkwe wa kigogo mmoja wa polisi ambaye ameishastaafu. Je hii haiwezi kuwa clue ya kutufikisha kwa Lugumi mwenyewe? Kutelekezwa na kutotekelezwa mradi mzima ni hasara kubwa kwa taifa kifedha na kiusalama.
Je ni makosa mangapi ambayo serikali ililenga kumpambana nayo yalitendeka baada ya Lugumi kutofunga vifaa husika?
            Mbali na Lugumi, kuna kashfa nyingine ambayo nayo ni tata; na ililisababishia taifa hasara ya mabilioni ya shilingi sawa na kashfa tajwa hapo juu. Kashfa hii si nyingine bali ya utwaliwaji wa iliyokuwa Kampuni ya Uchukuzi Dar Es Salaam (UDA). Kwa wanaojua historia ya kashfa hii ni kwamba UDA ilitwaliwa na kampuni ya Simon Group kinyume cha sheria na kwenye mazingira yenye utata kuhusiana na namna kampuni ilivyouzwa huku serikali ikikana kuwa hisa zake zilikuwa bado kuuza hisa zake. UDA ilikuwa ikimilikiwa na Halmashauri ya Jiji na serikali kwa uwiano wa hisa 49 (Serikali) kwa 51 (Jiji la Dar Es Salaam). Ajabu ya maajabu hata hisa za Jiji hazionyeshi namna zilivyouzwa. Hakuna ushindani uliofanyika kama sheria ya manunuzi ya umma inavyotaka. Je ni kwanini utaratibu ulikiukwa? Kama Lugumi, mmilki wa Simon Group, Simon Kisena ni mtu wa kutia shaka ambaye hana historia inayoeleweka kibiashara ukiachia mbali kutuhumiwa kuhujumu viwanda vya usindikaji pamba ambao ulimlazimisha rais Magufuli kutoa amri virejeshwe kwa umma huko mkoani Mwanza. Je, kama Lugumi, Kisena ni wakala wa wakubwa au jamaa zao ambao hawataki kujulikana? Hapa napo kunapaswa kufanyika uchunguzi kujua kilichoko nyuma ya pazia kama ilivyo kwa Lugumi.
            Kwa vile rais Magufuli amepania kurejesha uwajibikaji na heshima katika utumishi wa umma ikiwamo kuhakikisha mali na raslimali za umma zinaunufaisha umma, tunaamini kuwa ni wakati muafaka kumkumbusha kuwa na kashfa tajwa zishughulikiwe ili taifa lisiendelee kuchezewa na kuhujumiwa kiasi cha kujidhalilisha kwa kuombaomba na kutegemea uhisani wenye masharti magumu udhalilishaji vya hali ya juu. Kwani, haiingii akilini taifa liendelee kutoa huduma muhimu kwa umma wakati linaachia mali na raslimali zake kuhujumiwa na kundi dogo la mafisadi na wezi. Kazi ya serikali yoyote duniani ni kuwalinda wananchi wake na mali na raslimali zao. Isitoshe, serikali inavyo vyombo na asasi za kuweza kushughulikia kadhia kama hizi ambavyo watumishi wake wanalipwa mabilioni ya shilingi ya kodi za wananchi. Kama vyombo hivi na serikali wanashindwa na genge dogo la wachache, nini maana ya kuaminiwa na kulipiwa na umma?
            Tumalizie kwa kumtaka rais Magufuli na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) wajielekeze kwenye kadhia hii ili kuepusha upotevu wa fedha za umma ukiachia mbali uhujumu wa taifa. Kama alivyowahi kusema rais Magufuli, wakati wa Tanzania kuwa shamba la bibi umekwisha. Hivyo, Lugumi na Simon Group wanapaswa kuunganishwa na wenzao wa Escrow ili haki itendeke kwa pande zote ukiachia mbali kuonyesha seriousness ya rais Magufuli ya kupambana na uoza. Kwa leo tunaishia hapa.

Kijiwe kwenda Ukonga kuwasalimia akina Escrew

Sunday 23 July 2017

Wiki hii namkumbuka shujaa wangu Mahlathini

Sinon "Mahlathini" Nkabinde wiki hii anatimiza miaka 18 tangu atutokea kiroho ingawa kimwili daima atakuwa nasi kama si kupitia kwenye imani basi kwenye kazi yake. Tokana na kuwa mpenzi na shabiki mkubwa wa Mahlathini na Mahotela Queens huwa kila mwaka naadhimisha maisha ya nguli huyu wa muziki aliyetikisa anga la muziki hasa kwenye zama za ukaburu kiasi cha kuwa sehemu mojawapo ya ukombozi wa Afrika Kusini. Ni bahati mbaya kuwa ni mwezi huu wa Julai ambapo nguli mwingine David Masondo wa Soul Brothers alifariki ghafla miaka miwili iliyopita.

Magufuli atafanikiwa kutumikia mabwana wawili?

Image result for photos of magufuli kikwete and mkapa
            Akiwa ziarani mkoani Geita rais John Magufuli alisikika akilalamika na kuwataarifu wananchi namna baadhi viongozi wa ngazi za juu waliomtangulia walivyokuwa wameiuza Tanzania kwa kuwekewa chao kwenye mabenki huko Ulaya kama alivyosema. Kwa wanaojua namna Tanzania ilivyozamishwa kwenye ufisadi na uhujumu vya kutisha baada ya baba wa taifa Mwl Julius Nyerere kuachia ngazi wanajua aliowalenga Magufuli.  Alisema “mimi ni Yohana ninayeandaa njia… ndiyo maana nimejitoa… kwani mimi si ningeweza kuwekewa changu Ulaya? Hapa bila shaka wote waliohusika wanajulikana na kujijua ingawa wengine wanajitahidi kumkubali na kumsifia kwa kuanza kusafisha nchi waliyoichafua.  Hata hivyo, wapo wanaoanza kuhoji ithibati ya Magufuli hasa baada ya kutamka hadharani kuwa baadhi ya watangulizi wake wanaotuhumiwa kujihusisha na hujuma na ufisadi huu waachwe wastaafu kwa amini badala ya kufikishwa mahakamani; kama ambavyo baadhi ya watanzania walimtaka afanye. Je hii inaleta picha gani kuhusiana na ithibati ya Magufuli katika kutenda haki bila upendeleo?
            Magufuli aliongeza kuwa kwa kuogopa kufanyiwa hila, hataki kusafiri. Anakaa nchini ikuwatumikia wananchi.  Alikaririwa akisema “ndiyo maana sitembei, nikienda huko watafanya ya ajabu, ngoja nidili na nao kwanza, lazima nihakikishe nasafisha kwanza.” Hii inaonyesha kuwa Magufuli anaongoza nchi peke yake. Maana, kama ingekuwa si hivyo, basi asingehofia kusafiri. Pia, hii inaonyesha Magufuli hawaamini wasaidizi wake; na wala hawapi fursa ya kumsaidia. Maana kama angekuwa anawaamini asingehofia kutokuwapo kwake tena kwa siku chache kungesababisha hujuma. Hii maana yake ni kwamba wasaidizi wa rais wapo pale bila imani ya bosi wao. Pia, hii inaonyesha kuwa wasaidizi wa Magufuli hawana wanachomsaidia zaidi ya kuziba nafasi tu na kupokea mishahara na marupurupu bila sifa ya kuweza kumsaidia kuutimikia umma.
            Wakati akiyasema haya, Magufuri kabla ya hapo alikuwa amekaririw akiwataka watanzania kuwaacha marais wastaafu wapumzike; kwani walifanya kazi kubwa mojawapo ikiwa ni kumwezesha kufikia alipofikia. Je hili ni jambo la kujisifia na kuwasifia wahusika au Magufuli anawapiga vijembe kuwa uzembe wao ndiyo umemfikisha hapo alipo kama rais tena mwenye kusifika dunia nzima kwa kusafisha uoza hata kama ni kwa upendeleo? Maana, haiwezekani Magufuli akasema wapo viongozi wa umma wa juu waliouza nchi halafu hapo hapo akawasifia akaeleweka. Anasema marais wastaafu walifanya kazi kubwa. Kazi ipi; kama mambo yenyewe ni haya? Je Magufuli anaanza kujipiga mtama kiasi cha kujichanganya? Je kati ya uzalendo na ufisadi, Magufuli atachukua njia ipi? Je uoza alioukuta unavumilika au kuweza kukingiwa kifua; au kutafsiriwa kama kazi kubwa waliyofanya watangulizi wake? Je Magufuli anaanza kugundua makosa aliyofanya kwa kutoa matamko ya kuwalinda watu waliofanya uovu huku akijua hili linapingana na dhamira yake ya kweli ya kulikwamua na kulikomboa taifa hili lililokuwa limegeuzwa shamba la bibi kama ambavyo amekuwa akisema mara nyingi? Je Magufuli atatenda miujiza gani kufuta kauli kama hizi na kufanya kinyume chake kwa kuhakikisha kila aliyeshiriki uchafu anafikishwa mbele ya vyombo vya dola? Je, kisheria, rais anao uwezo wa kumsamehe mtu makosa ya jinai kabla ya kupatikana na na hatia akafungwa ndipo akamuachia kwa msamaha wa rais?
             Je Magufuli ataweza kuendelea kuwalinda wastaafu wanaotuhumiwa huku akiwaumbua hadharani kama alivyofanya akiwa Chato tena wengine wakiwapo baadhi yao? Je itawekezekana Magufuli kuwatumikia wanyonge kama asemavyo mara kwa mara sambamba na kuwahifadhi waliowaibia wazi wazi? Kwanini Magufuli asiwaache akina Benjamin Mkapa, Jakaya Kikwete n ahata Ali Hassan Mwinyi wakabeba mizigo yake wakati yeye akibeba jukumu la kuuondoa umma kwenye uoza na kero walizotengeneza wawili hawa bila sababu za msingi zaidi ya ufisadi na uroho wa kawaida tu? Nani hajui kuwa watanzania bado wanafahamu namna Mwinyi alivyohalalisha ufisadi kupitia sera yake ya ruksa. Nani hajui Mkapa alivyofanya biashara akiwa ikulu kinyume cha sheria? Rejea makampuni yake kama vile ANBEM lenye kuundwa na ufupisho wa Mkapa na mkewa Anna, Tanpower na Fosnik kampuni ya mwanae inayoundwa kwa majina yake yaani Nicholas na Foster. Rejea kujitwalia machimbo ya Makaa ya Mawe ya Kiwira kinyume cha sheria na kashfa nyingine kama vile kuhujumu shirikala la umeme la Taifa (TANESCO) na iliyokuwa Benki ya Biashara (NBC).
            Tukija kwa Kikwete, watanzania wanajua namna alivyoshirikiana na Mkapa kwenye kashfa ya EPA ambayo wanaojua ukweli wanasema wazi ilivyompa mtaji wa kupatia urais. Kikwete haishii hapa. Nani amesahau kashfa yake ya Richmond ambayo ilimlazimisha kumtoa kafala rafiki na waziri wake mkuu Edward Lowassa mbali na mauza uza mengine kama vile utwaliwaji wa lilokuwa Shirika la Usafiri Dar es Salaam (UDA) kati ya nyingi? Je Magufuli atatumia miujiza gani kuwasahaulisha watanzania uchafu huu ili waendelee kumwamini na kumuunga mkono kwenye harakati zake zinazoanza kuharibiwa na hii hali ya kuwakingia kifua watawala wa zamani waliotuhumiwa kujihusisha na ufisadi? Je hapa Magufuli anapigana vita na ufisadi gani kama hawezi kuwaacha kila mtu abebe mzigo wake? Je vita ya ufisadi nchini itafanikiwa kwa kuwasulubu dagaa na kuwakumbatia mapapa na bado iendelee kuleta maana kiasi cha kuendelea kuwashawishi watanzania kuwa ni kwa ajili yao hasa wanyonge?
            Tumalizie kwa swali. Je rais Magufuli atafanikiwa kutumikia mabwana wawili?
Chanzo: Tanzania Daima J'pili leo.

Je ni kweli Magufuli anapanga kuiba kura Kenya?


Saturday 22 July 2017

Kwa Weekend faidi hii kitu


Wanaopinga si wapumbavu bali wasiotaka kupingwa

Juzi walevi tulipigwa na butwaa. Si baada ya muishiwa mlevi mkubwa wa ulaji kupayuka kuwa sisi tunaopinga–mambo yanapokwenda ndiyo siyo–eti ni wapumbavu! Kama siyo kukaza roho, huenda hali ingekuwa tofauti baada ya walevi wote kushika michupa yao na kuingia mitaani kutaka tubadili katiba na kuondoa kinga kwa viumbe kama hawa wasiojua kuwa bila sisi wao si lolote si chochote. Tunawalisha, kuwavika, kuwatibia ughaibuni na anasa za kila aina dunia bure tena kwa kazi bure waliyofanya japo si wote halafu wanatutapikia hivi. Shame on you Dugong Makapi. Kama siyo upumbavu, hapa upumbavu wa walevi uko wapi?
            Baada ya kuinyaka kwenye runinga namna jamaa alivyopayuka, nilijikuta nikisema “how dare you Dugong?”  Jamaa huyu Tunituni mwenye uvivu wa kufikiri aliudhika kusikia eti baadhi ya walevi wanampinga kaisari anapozidisha mambo. Kwa wenye akili na hekima na si wajivuni, malimbukeni na wavivu wa kufikiri, kukosoana, licha ya kuwa chemi chemi ya maarifa, ni ustaarabu wa hali ya juu uliojikita kwenye demokrasia; ni uwazi hasa katika kuendesha mambo ya kaya. Anayetaka asikosolewe asijiingize kwenye utumishi wa umma na aache upumbavu wa kuona wanaomkosoa kuwa maadui au wapumbavu.  Hivi kweli kukosoa ni upumbavu kweli?  Nadhani upumbavu ni kutokubali kukosolewa hasa tukizingatia kuwa ni Mungu pekee asiyekosolewa. Binadamu ana nini cha mno hadi asikosolewa; wakati kila sekunde ipitayo hutenda madhambi na kukosea?
             Natoa tahadhari mapema. Msitake kututia madole mkadhani hatujui madhambi yenu. Nani alijua kuwa waungwana kama Luis Inacio Lula da Silva aliyeifanyia makuu Brazil angeburuzwa kwa pilato? Kama kuchokoana dili, chokochoko kanchokoe pweza; ila si walevi watakatifu na wachapa kazi wanaolisha kila aina ya kupe kayani.
            Kifalsafa, binadamu ni kiumbe dhaifu kuliko hata wanyama; ila amewazidi kwa sababu ya sanaa ya mawasiliano ambayo sasa wengine wanaanza kuitukana kwa kuitumia vibaya kama huyu mlevi mkubwa aliyejivua nguo hadharani na kuonyesha alivyo mbumbumbu wa demokrasia. Muishiwa huyu mkubwa bingwa wa kutukana walevi wapumbavu asijiangalie sana. Tatapinga pale tutakapoona tunaburuzwa kama kutaka tuwasamehe wezi na majambazi wakubwa waliotumia ofisi zetu kujinufaisha; wakati sisi tukimenyeka bila sababu zaidi ya upumbavu na uroho vyao. Mfano mdogo, ni pale kaisari alipotuasa tuwaache mafisadi wakubwa waliotuuza kwa wachukuaji wapumzike wakati walituibia mmojawapo akiwa huyu aliyeonyesha umamuma wake wazi wazi. Go tell it to the birds; lazima wasulubiwe. Pia, waachwe wabebe misalaba yao kama alivyosema mwana wa Adam kuwa kila mtu atauchukua mzigo wake mwenyewe.
            Mjivuni huyu na mvivu wa kufikiri amesahau kuwa tunayajua machafu yake kuanzia unyakuzi hadi uvivu wa kufikiri hadi akazidiwa kete na bi nkubwa aliyemuingiza kwenye umachinga akiwa patakatifu pa patakatifu. Kama upumbavu wetu ni kumvumilia, basi patachimbika bila jembe. Mbona muishiwa huyu hataki kujifunza yaliyojiri hivi karibuni kule kwa walevi wa Korea ya Kusini na Brazil ambapo walaji wakubwa mmoja alihukumiwa miaka tisa na ushei; huku mwingine akinyea debe. Anadhani sisi ni mabunga yasiyobadilika au mawe? Akome na kukomaa.
            Huyu dingi hajui kuwa tunajua anavyotuingiza hasara kwa kulipwa mabilioni ya njuluku wakati alipaswa awe Ukonga akifanyia kule vitu vyake na wenzake kama akina Seti na Rugetumbuliwa; kama siyo akina Hasi Kiti… Hakuna ukumbaff kupita kiasi kama kujisahau; na anayefanya hivyo akadhani wote tumesahau. Tunakumbuka Kiwila, ANbeni, Tanpawa, NBC, Fosiniki EOTf na maulaji mengine mengi aliyoasisi na kutupiga njuluku zetu ukiachia mbali uwekezaji wa kichukuaji na kijambazi. Ni bahati mbaya kushindwa kujua kuwa aliyeko juu mngoje chini au ikizidi mpandie. Hajui kuwa walevi tunaweza kumpandia na akaishia kubwagwa chini bila kutarajia? Bora azibe domo lake chafu kabla hatujamshukia ili apatilizwe na kusulubiwa kwa madhambi yake.
            Buda huyu au dingi, kama wasemavyo manyang’a, bingwa wa kupayuka amesahau kuwa zake zilikwisha zamani kiasi cha kuishi akitegemea kukingiwa kifua na kaisari junior kwake ili tusimfikishe kwa pilato akanyolewa bila maji. Kama amesahau au anajisahaulisha, namshauri asome waraka huu tena aukariri ili akijisahau uwe unamkumbusha kuwa walevi si wakumbaff, hawajawahi kuwa wakumbaff wala hawatakuwa wakumbaff kama yeye. Mijitu mingine bwana kwa kujisahau, yaani jamaa limesahau lilivyomhangaisha mzee wetu Musa kulipigia ndogo ndogo zama za kinyago cha mpapure! Ama kweli ukishangaa ya tumbili utaona ya nyani! Na ama kweli nyani haoni nonihino lake. Nimalizie. Walevi wapingaji si wapumbavu bali upumbavu ni kutokutambua mchango wao na ukweli kuwa kukosoana ni demokrasia na ustaarabu. See you next week guys.
Chanzo: Nipashe Jumamosi leo.

Wednesday 19 July 2017

IPTL is not a grave – it’s a massive graveyard

Currently, I hear jubilations everywhere as the Tanzanians sing praise of their political newbie hero, President John Pombe Magufuli; for pluckily hoofing it where most of his predecessors feared to. This is because the hoi polloi were betrayed and demoralised for many years, since Mwl Julius Nyerere’s abdication. This said; it isn’t hard to gauge how graft had dangly secured conviviality with the politicos so as to become a furtive policy before Magufuli’s arrival. After striking two individuals Havinder Sethi Singh and James Rugemalira–whose cases we can’t discuss; because they’re before the court–hoi polloi seem to be enchanted. Essentially, these vandals along with public venal officials, are the architects, or call them the black boxes if not a cockpit of the ever-lossmaking investment, the Independent Power Tanzania Limited (IPTL) by which the national lost about US$200 million pointlessly. Taking on such stinking graft is no mean feat; though we need to courageously turn more big stones.
            Demonstrably, the IPTL isn’t a grave but a graveyard. Thus, this is the beginning in that Escrow shouldn’t undercut the doggedness to attach IPTL. Instead, it must undergird the interests of the citizenry but not a select few.
In dealing with this imp, there are so many unknown things that need to be known. For example, how do you deal with Escrow scam without dealing with its mother, the IPTL, which enabled hoaxers to rob our nation? My source confided me; Singh and Rugemalira jointly own just 50% shares of the IPTL; and the rest is owned by a mysterious creature[s], Simba Trust. Who is [are] Simba Trust that’s never been divulged since the scam came to the fore? We need to know them.
            I heard that the government attached the chattels the accused and suspects that are still at large own. Does this include Tageta IPTL plant that’s, apart from polluting our country, been used in milking the Tanzania National Electric Company (TANESCO) day in and day out; not to mention causing power hike for unsuspecting and always sheepish consumers? Again, arresting the culprits is an easy part of the mêlée against graft committed with impunity. Are we legally prepared to prosecute all players in this leech without knowing them all? What are suspects that are still in public offices or position such as members of parliament waiting for?
            According to an out-front anti-graft crusader and researcher who did a lot about exposing the scam, the “IPTL begat Escrow” and the two are one like yin and yang. Further, he maintains that the IPTL profligacy didn’t only caused the losses of millions of dollars but billions; if we consider the its negative effects on the economy and individuals who picked up the tab. He bases his assertion to the fact that when our venal biggies, harranguedly, ‘blessed’ the IPTL for their personal ends, Tanzania lost many international financial grants among which is USD473m US Millennium Challenge Account grant that would have financed new power projects in the country.
            A little bird confided me that the IPTL has dented private power plants (IPPs) (which are cost effective) due to its ravenousness and duplicity.  Sadly though, not all Tanzanians know that the cheapest IPP in Tanzania, Songas, for 13 years, has been selling power to TANESCO for less than 6 US cents per kilowatt-hour, while TANESCO hikes it to its customers for about 12 US cents. According to a 2013 report by the President's Delivery Bureau, IPTL’s power cost TANESCO 24 US cents while Symbion’s and Aggreko’s emergency power projects cost up to 42 US cents despite the fact that the Government, through TANESCO, TPDC and TDFL, owns over 40% of Songas’s shares apart from receiving dividends from Songas in addition to the relatively low-cost power. Aren’t these deadly, lossmaking and toxic investments?
             To cut a long story short, if indeed, Tanzania is deadly serious and it aims at doing away with such shoddy and toxic investments, must see to it that the IPPs are supported even by using the monies it has been burning on criminal investments such as the IPTL, Symbion aka Dowans aka Richmond former venal regime ushered in to restively ruin our economy.
Source: Citizen Wed., today.

Tuesday 18 July 2017

Leo Tumetimiza miaka 19 ya Ndoa



Kwa ndugu jamaa na marafiki, leo mimi na mke wangu Nesaa tumetimiza miaka 19 tangu tufunge ndoa. Katika kusherehekea siku hii  muhimu kwetu, pia huwa tunakumbuka kuwa ni siku ya kuzaliwa kwa shujaa wetu Nelson Mandela-ambaye kama angekuwa hai leo-angetimiza miaka 99. Tumefurahia keki na kadi tulizonunuliwa na watoto wetu kila mmoja akieleza anavyojihisi kuwa wazazi wake ukiachia mbali Nkwazi Jr na Nkuzi ambao hawajui kuandika. Kwetu ndoa si ndoana bali shule na pepo. Tunazidi kumshukuru na kumuomba Mungu aendelee kutupa na kutujalia amani upendo na utulivu tangu mwanzo wa safari yetu. Tunazidi kushukuru kuwa upendo wa kweli na wa ari si kiungo ambacho kiliwahi kupungua au kukosekana tangu mwanzo wa safari yetu. Si hayo tu, tunamshukuru Mungu kwa kutujalia wana na mabinti si haba ukiachia mbali furaha na kufaana visivyo vya kawaida. 


Baada ya Escrow Lugumi na UDA nao watumbuliwe

Image may contain: 1 person, smiling, standing                        Hivi karibuni rais John Magufuli aliwafurahisha watanzania kiasi cha kuwaaminisha kuwa ufisadi hauna nafasi katika nchi yetu. Ni baada ya kuchukua hatua za makusudi na za kupongezwa za kuwakamata na kuwafikisha mahakamani watuhumiwa wa kashfa ya wizi wa mabilioni ya fedha toka kwenye fuko la Escrow. Kimsingi, hatua hii adimu na adhimu ilizidi kuongeza imani ya umma kuwa kumbe hakuna asiyeguswa japo bado wapo marais wastaafu ambao serikali zao ziliingiza kampuni la Independent Tanzania Power Limeted (IPTL) ambalo ndiyo mama wa wizi na uhujumu huu.
            Tokana kuanza kuishughulikia kashfa ya Escow kisheria, wengi wanaamini mwisho wa yote mkono mrefu wa sheria utatua IPTL. Pamoja na hatua hii ya kutia moyo, wengi wangetaka rais Magufuli aende mbali na kuwakamata watuhumiwa wengine ambao walihujumu taifa na kuliingiza hasara ya mabilioni ya shilingi. Leo, bila kuficha wala kumung’unya, tunamkumbusha rais Magufuli kuwa bado kuna kashfa nyingine kama vile Lugumi ambapo kampuni iitwayo Lugumi Enterprises Limited inadaiwa kupewa tenda na jeshi hilo kwa ajili ya kufunga mashine za kuchukua alama za vidole – ‘Biometric Access’ katika vituo 108 nchi nzima kwa gharama ya Sh bilioni 37. Mpaka kashfa yenyewe inaibuka Lugumi iikuwa imefunga mashine katika vituo 14 pekee wakati ilikuwa tayari imeishalipwa Shingili bilioni 34 ambazo ni sawa na asilimia 99 ya fedha zote za mkataba. Kuna haja ya kuchunguza mazingira na sababu za kufanyika kwa malipo haya kwa kampuni ambayo ilikuwa haijafanya kazi yoyote ukiachia mbali kuchunguza historia ya kampuni ya Lugumi na wamilki wake.
Image result for simon kisena pichani
            Je, kama hakukuwa na namna, ilikuwaje kampuni hiyo ikapewa malipo ya asilimia 99 bila kuwa imetekeleza angalau asilimia sawa za kazi iliyokuwa iifanye? Maana, kiakili na kisheria ni jambo lisilowezekana bila kuwa na namna yoyote haramu ya kupinda au kuvunja sheria. Je Lugumi ni kikaragosi kilichotumiwa na wakubwa fulani kuliibia taifa?
            Kuna taarifa ambazo hazijawahi kupingwa kuwa Lugumi ni mkwe wa kigogo mmoja wa polisi ambaye ameishastaafu. Je hii haiwezi kuwa clue ya kutufikisha kwa Lugumi mwenyewe? Kutelekezwa na kutotekelezwa mradi mzima ni hasara kubwa kwa taifa kifedha na kiusalama.
Je ni makosa mangapi ambayo serikali ililenga kumpambana nayo yalitendeka baada ya Lugumi kutofunga vifaa husika?
            Mbali na Lugumi, kuna kashfa nyingine ambayo nayo ni tata; na ililisababishia taifa hasara ya mabilioni ya shilingi sawa na kashfa tajwa hapo juu. Kashfa hii si nyingine bali ya utwaliwaji wa iliyokuwa Kampuni ya Uchukuzi Dar Es Salaam (UDA). Kwa wanaojua historia ya kashfa hii ni kwamba UDA ilitwaliwa na kampuni ya Simon Group kinyume cha sheria na kwenye mazingira yenye utata kuhusiana na namna kampuni ilivyouzwa huku serikali ikikana kuwa hisa zake zilikuwa bado kuuza hisa zake. UDA ilikuwa ikimilikiwa na Halmashauri ya Jiji na serikali kwa uwiano wa hisa 49 (Serikali) kwa 51 (Jiji la Dar Es Salaam). Ajabu ya maajabu hata hisa za Jiji hazionyeshi namna zilivyouzwa. Hakuna ushindani uliofanyika kama sheria ya manunuzi ya umma inavyotaka. Je ni kwanini utaratibu ulikiukwa? Kama Lugumi, mmilki wa Simon Group, Simon Kisena ni mtu wa kutia shaka ambaye hana historia inayoeleweka kibiashara ukiachia mbali kutuhumiwa kuhujumu viwanda vya usindikaji pamba ambao ulimlazimisha rais Magufuli kutoa amri virejeshwe kwa umma huko mkoani Mwanza. Je, kama Lugumi, Kisena ni wakala wa wakubwa au jamaa zao ambao hawataki kujulikana? Hapa napo kunapaswa kufanyika uchunguzi kujua kilichoko nyuma ya pazia kama ilivyo kwa Lugumi.
            Kwa vile rais Magufuli amepania kurejesha uwajibikaji na heshima katika utumishi wa umma ikiwamo kuhakikisha mali na raslimali za umma zinaunufaisha umma, tunaamini kuwa ni wakati muafaka kumkumbusha kuwa na kashfa tajwa zishughulikiwe ili taifa lisiendelee kuchezewa na kuhujumiwa kiasi cha kujidhalilisha kwa kuombaomba na kutegemea uhisani wenye masharti magumu udhalilishaji vya hali ya juu. Kwani, haiingii akilini taifa liendelee kutoa huduma muhimu kwa umma wakati linaachia mali na raslimali zake kuhujumiwa na kundi dogo la mafisadi na wezi. Kazi ya serikali yoyote duniani ni kuwalinda wananchi wake na mali na raslimali zao. Isitoshe, serikali inavyo vyombo na asasi za kuweza kushughulikia kadhia kama hizi ambavyo watumishi wake wanalipwa mabilioni ya shilingi ya kodi za wananchi. Kama vyombo hivi na serikali wanashindwa na genge dogo la wachache, nini maana ya kuaminiwa na kulipiwa na umma?
            Tumalizie kwa kumtaka rais Magufuli na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) wajielekeze kwenye kadhia hii ili kuepusha upotevu wa fedha za umma ukiachia mbali uhujumu wa taifa. Kama alivyowahi kusema rais Magufuli, wakati wa Tanzania kuwa shamba la bibi umekwisha. Hivyo, Lugumi na Simon Group wanapaswa kuunganishwa na wenzao wa Escrow ili haki itendeke kwa pande zote ukiachia mbali kuonyesha seriousness ya rais Magufuli ya kupambana na uoza. Kwa leo tunaishia hapa.
 Chanzo: Tanzania Daima Jumatano kesho.

Kijiwe kwenda Ukonga kuwasalimia akina Escrew

          Leo Mgoshi Machungi amekuja na mpya. Si alikishangaza kijiwe aliposema kuwa alikwenda Keko kumuona Mgoshi Semtwashua na kuambiwa kuwa wale watuhumiwa wa Escrew wanaishi kwenye vyumba vya VIP lupango.
            Baada ya kuamkua anakula mic “wagoshi jana niishangaa sana.” Kabla ya kuendelea Mbwamwitu anadakia “kwani ulikwenda feri au bandari kushangaa namna vichwa 15 vinavyoweza kuingia na kupakuliwa bandarini bila kujulikana mwenyewe? Au ulikuwa chumbani ambako maji huingia sehemu na kugeuka kiumbe? Si ulisikia juzi namna watasha walivyotengeneza kondoo Dolly kwenye chupa tena kwa kutumia maji ya nonihino?”
            Mgoshi anajibu “hii hainishangazi hasa tikizingatia kuwa bado tina watu wanaodhani kuwa Dokta Kanywaji hawezi kuwatumbua kama aivowafanyia akina Eskoo ambao hata hivyo niiambiwa kuwa wanaisha kwenye vyumba vya VIP wakitanua kama vie hawako upango.”
            Kapende anampoka Mgoshi mic “ina maana Dokta Kanywaji amezidiwa ujanja na ndata wa lupango au ni uzushi wa kawaida? Nitashangaa na kusikitika kama habari hizi zitakuwa za kweli. Ama kweli ukishangaa ya Escrew utaona ya IPTL! hata hivyo, nani ajuaye? Lolote lawezekana kwenye kaya hii ya maajabu.”
            Kabla ya kujibu Kanji anakwanyua mic “na mimi iko sikia toka vatu yangu ya karibuni kuva ile vatu ya escrew naishi kama iko jumbani yao. Iko moja naambia mimi kuva napelekewa hata bibi kuburudisa yeye. Hii kaya iko complications mingi dugu yangu. Mimi ikodhani kuwa Svahili sana nagombea ile Singasinga kama bwabwa.”
            Kabla ya kuendelea mzee Maneno anamchomekea “hii kweli kali! acha ndugu yangu Kanji nikuchomekee. Mana sikuelewi. Unamaanisha nini unaposema kuwa Swahili nagombea Singasinga kama ubwabwa? Sasa kama napelekewa bibi kwanini isigombee hiyo bibi badala ya kugombea Singasinga au wanagombea yote kiasi cha Singasinga kulalamika kuwa haipati singizi tokana na hofu kama vilivyoripoti vyombo vya umbea hivi karibuni?”
            Kabla ya kujibu Mpemba anajibu “hapa mie ndhani huyu aongelea yale mambo ya Popobawa. Maana, nasikia haya mambo yako sana kule ati. Kwani yeye nani asiliwe? Mie ningependa nisikie kuwa nao yakhe waliwa kama walivokula njuluku zetu wallahi.”
            Mijjinga anakatua mic “mie Singasinga hanipi taabu. Nitasherehekea na kuwamwagia ofa ya kahawa kama nikisikia kuwa na Nshomile Rugetumbuliwa naye anashikishwa ukuta. Kwanini wao watutese wasiteseke? Kwanini wale vyetu vyao visiliwe? Natamani ningekuwa kule niwasheherehekee kama walivyosherehekea njuluku zetu.”
            Mchunguliaji anachomekea “mbona wanashikishwa ukuta sana kila wakitoka na kuingia. Mie nayajua maisha ya lupango. Ukitoka kwa pilato unavuliwa nguo zote ili kuhakikisha huiingii na mabomu kama vile bangi, fedha na mambo mengine. Jamaa kule wana laana ile mbaya. Wanakupekuwa kila mahali tena ukiwa uchi wa mnyama. Hivyo, kushikishwa ukuta wala si ajabu wala adhabu. Ni utaratibu wa kawaida.”
            Msomi Mkatatamaa aliyekuwa akibukua jarida moja la kimataifa liitwalo Corrupt Poor Countries anakula mic “Mtu binafsi akiliwa siyo real deal. Kama wao walituibia, kuna kosa gani yakawakuta haya? Hata hivyo, dua la kuku halimpati mwewe.  Kama alivyosema Mgoshi na Kanji, intelligence yangu inaniambia kuwa hawa jamaa wanaishi kama wako uraiani hasa ikizingatiwa kuwa wana njuluku ya kuhonga na kupewa upendeleo. Kama bangi na simu za mkononi zinapenyezwa, watashindwa kuhonga na kupewa upendeleo hasa ikizingatiwa kuwa kwao njuluku ambao hawakuzitolea jasho si tatizo. Sitashangaa kukuta madai haya ni ya kweli hasa ikizingatiwa kuwa bado kaya yetu ina ufisadi ambao umegeuka donda ndugu. Kinachofurahisha ni kwamba angalau Dokta Kanywaji amethubutu waliposhindwa wengi kiasi cha kuwatia kiwewe hadi wakamfuata kwake kumramba makalio kama alivyofanya Tunituni Makapi hadi akapayuka kuwa wapingaji ni wapumbavu asijue naye ni wale wale.”
            “Msomi usinikumbushe fisadi huyu mjivuni ambaye, hata hivyo, vyombo vya umbea havikumlazia damu zaidi ya kumpa kavu kavu aache upumbavu na upayukaji asijeishia walikoishia wenzake wa Brazil na Korea ya Kusini hivi karibuni walipofikishwa mbele ya haki bila kutarajia,” anachomekea Mipawa huku akiendelea kufyonza kipisi chake cha sigara kali.
            Mheshimiwa Bwege aliyekuwa akisikiliza kwa makini anaamua kutia guu “mie mpaka sasa sina imani na mazingaombwe na sanaa zinazoendelea mbele ya mapilato hasa kutokana na kuachiwa na wale jamaa wa Bandarini ambao walipiga wazi wazi wakaishia kuchomoka. Sijui walitembeza chochote kitu au waliowanasa hawakufanya homework yao vizuri. Maana system sasa inaonekana bwege na cha mtoto kiasi cha kuwadaka mafisadi wakachomoka kirahisi. Je hapa tatizo liko wapi au kuna namna mapilato nao wanafanya kama siyo mandata wanaochunguza kesi husika?”
            Sofia Lion aka Kanungaembe anakwanyua mic “kaka lolote linawezekana. Unategemea nini mapilato wanapokuwa kama yule aliyekwanyua njuluku za Escrew aliyelazimishwa kutema ulaji hivi majuzi? Sijui naye ataunganishwa na akina Bill Gereza na Endelea Chenga na profwedheha Anae Kajuamlo kwenda lupango lau kufanya vitu vyao kwenye mtondoo?”
            Kijiwe kikiwa kinaendelea si likapita shangingi la Bashite? Acha tumzomee tukitaka naye apelekekwe lupango kwa kughushi.
Chanzo: Tanzania Daima Jumatano kesho.