The Chant of Savant

Thursday 4 December 2014

Mkiwa na watawala hamnazo matatizo matupu!


Waziri wa Fedheha, sorry Fedha, Saada Mkuya akisaini mkataba wa makabidhiano ya shilingi bilioni 45  na mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo la Saudi Arabia Hassan al Attas jijini Dar. Inashangaza nchi inavyoomba omba na kukopa lakini bado ikaruhusu ufisadi wa kutisha kama vile wa escrow. Je hii misaada tunayopewa ni misaada au kuna mengine nyuma yake? Kwanini hawa wanaotoa misaada kama wana nia nzuri wasiulize hizi tunawamwagia mafisadi kwanza? Je wanatumia udhaifu wa utawala wetu kujipenyeza watuumize baadaye? Inakuwaje Saudia watoe msaada wa kifedha hata kabla ya wafadhili hawajatoa tamko kuhusiana na kashfa ya escrow iliyowafanya wagome kuchangia shilingi bilioni moja kwenye bajeti ya taifa? Je Saudia inaanza kupingana na wafadhili? Ili iweje? Maswali ni mengi kuliko majibu.

2 comments:

Anonymous said...

Wakati tunaposoma historia za mababu zetu afrika. Tuliona kuwa mababu zetu walikuwa na ukosefu wa maarifa kielemu lakini walikuwa na akili timamu ya kutambua uzalendo kuliko, hawa wezi tuliyonao sasa.

Nyakati zote huwa na tafakari jinsi wale wanyama waliosafirishwa Kilimanjaro Airport walivyo-wakubwa vile hawakuonekana hata lile dege na ukubwa wote pia nalo halijaonekana pia.

Tunahangaika na Escrow lakini tunasahau waliosahini mikataba hiyo tena zaidi wengine wamepewa majukumu ya kuwa wakuu wa kaya.

Kama kweli tunataka kuondoa sumu kionagozi yoyote aliyeshiriki na takashiriki kusaini mikataba yenye kuleta uharibifu maisha na raslimali ya Tanzania wanatakiwa kuhukumiwa kunyongwa.

Kwa sababu mikataba ni mngi hewa ya kitapeli kila siku na tunawachekea wahusika ndiyo sababu wanaendlea kuwapo na kuharibu vizazi vya wananchi wa Tanzania. Tena tulivyowapumbavu tunaweka hatima zetu za maisha mikononi mwao kwa kuwapa mamlaka kama vile kutnga katiba na hata kuongoza nchi. Eti tunategemea kupata maendeleo kutoka kwako lini yatatokea!

Hivi sasa tunaendelea kukupa kutoka kwenye mashirkia ya kimataifa Deni la taifa limekuwa mara tatu kabla ya serikali hii kuingia madarakani. Na sasa tunaota ndoto kwamba kugunduliwa kwa mafuta na gesi ndiyo jibu la matatizo ytu ya kiuchumi siyo kweli hili swala maana hivi sasa mafuta na gesi yanashuka bei siku hadi siku kwenye soko la dunia. Sababu mojawapo uzalishaji hupo juuu kuliko mahitaji.

Pia vyanzo mbadala vya nishati vimeongezeka, hivyo thamini ya mafuta na gesi itaendlea kushuka bei wakati deni la taifa litakuwa pale pale tena kuongezeka kwa riba iliyopo. Hivi itakuwa hivi mapaka lini Afrika??????

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Anon maneno yako mazito na ya hekima yakionyesha ngoa na usongo ulivyo navyo dhidi ya manyang'au wanaotutawala na kutula kama ujaka. Sitaki niharibu ujumbe wako zaidi ya kuungana nawe na kukushukuru kwa ujasiri na uoni wa mbali. Tunahhitaji watu kama wewe kulikomboa taifa letu tegemezi si kwa raslimali bali ukosefu wa viongozi wenye visheni hata common sense. Ubarikiwe sana na karibu tena na tena utoa mchango wako unaohitajika sasa kwa sasa.