The Chant of Savant

Tuesday 15 July 2014

Urais unapogeuzwa urahisi




BAADA ya urais kugeuzwa urahisi kiasi cha watu wa hovyo wasio na sifa (watimbwakwiri) wala mipango kuuwania kwa udi na uvumba, ni jukumu la Watanzania kuwa makini kwenye uchaguzi ujao.
Kutokana na tabia na mikakati inayojidhihirisha kwa sasa ambapo watu wasiofaa wanawania urais kwa kila njia ili watengeneze fedha na utajiri wa haraka, kuna haja ya kuwatahadharisha Watanzania, hasa wapiga kura, kuhakikisha wanatumia kura zao vizuri kuepuka kuitumbukiza nchi kwenye balaa jingine la utawala usio na visheni wala maadili isipokuwa madili.
Katika kufanikisha mipango yao michafu, wanaowania urais, wamejiandaa kutumia fedha chafu na haramu kuwahonga wapiga kura ili wapate urais na kuutumia watakavyo kutuibia.
Tumeishashuhudia watu wenye kutia kila aina ya shaka wakijipitisha na kujinadi. Tunawajua nao wanajijua fika. Wapo wanaowania urais kwa sababu tu ni watoto wa wakubwa wanaoweza kutumia mitandao ya kifisadi ya wazazi wao kufanikisha malengo yao.
Wengine wanawania urais kwa vile wana fedha chafu na ushawishi uliojengeka kwenye mambo ya hovyo kama vile kuhonga wana jamii wenye tamaa na wasioona mbali ili wawaunge mkono.
Baba wa taifa, hayati Mwalimu Julius Nyerere aliwahi kutuusia kuwa tuwaogope wanaokimbilia Ikulu kama ukoma. Na kweli sasa tunawaona wakijipanga vilivyo kutuingiza mkenge kwa mara nyingine.
Huwa najiuliza, kwa mfano, kijana ambaye amemaliza shule juzi juzi na kupewa madaraka ndani ya miaka mitano, eti naye anasimama anataka kuwa rais wetu kwa vile ana watu wanaomsukuma afanye hivyo. Ukimuuliza amelifanyia nini taifa zaidi ya kulihujumu kwa kupendelewa na nafasi ya mzazi au wazazi wake kufikia hapo alipo hana jibu la maana.
Kufanikisha njama za kutupandikizia rais ambaye atalinda uoza wa waliomtangulia na genge lao, wamebadili utaratibu mzima kuanzia daftari la wapiga kura hadi vigezo vya kumpata rais.
Haiingii akilini kwa mfano, kwa nchi yenye miundombinu hafifu kama umeme kuanzisha kile wanachokiita Biometric Voter Registration (BVR) ambayo mwaka jana tu ilisaidia watawala waovu kwenye nchi ya jirani kuiba kura na kupandikiza kibaraka wao kwenye ofisi ya rais.
Kama hakuna namna ya kuchakachua uchaguzi ujao, ni kwanini tunarudia makosa waliyofanya wenzetu huku tukiona yanavyowagharimu?
Kitu kingine kinachoonyesha wazi kuwa genge la watu wachache limejizatiti kuupoka urais tena ni ile hali ya viongozi kutotaja mali zao wala kusimamia maadili hasa wagombea kutaja utajiri wao na jinsi walivyopata hii fedha wanayomwaga kuhonga wajumbe kwenye vyama vyao ili wawapitishe ukiachia mbali kufuja fedha nyingi na nyingine kuanza kuibwa toka kwenye fedha ya umma. Hakika, haya ni maadalizi ya maangamizi ya taifa kama wapiga kura hawatakengeuka na kukomesha magenge haya yanayosaka urais.
Tangu ilipoanzishwa mitandao ya kifisadi ya kuusaka urais hapo mwaka 2005, wahusika wamezidi kuipanua ili waitumie kuupata urais na baadaye wajilipe kwa kuliibia taifa.
Zaidi ya tamaa ya madaraka na utajiri wa haraka, wengi wa wanaojitangaza kuutaka urais hawana hoja wala ajenda ya maana kwa taifa. Kama alivyoonya baba wa taifa, ni watu wa kuogopwa kuliko hata ukoma hasa ikizingatiwa kuwa Ikulu si patakatifu pa patakatifu tena kama ilivyokuwa zamani.
Kwa sasa Ikulu inavutia waroho wa madaraka hata wahalifu hasa ikizingatiwa kuwa imegeuzwa mahali pa kufanyia biashara na jinai nyingine.
Rejea kuzuka mtindo wa wake wa marais kuunda NGO’s zenye kila dalili za nyenzo za kusaka fedha ukiachia mbali watoto wa marais kuanza kujiingiza kwenye nafasi nono kisiasa ili kuendelea kutengeneza utajiri haraka.
Hapa hujaongelea marafiki wa wale wanaofanikiwa kuupata urais wanaoajiriwa au kuteuliwa kwa sababu moja tu, uwenzetu, ushirika au kulipana fadhila.
Tumeshuhudia baadhi ya waandishi wa habari waliotumiwa kuwachafua baadhi ya wanasiasa kisha baada ya hapo wakapewa vyeo vikubwa. Mitandao hii tajwa inakwenda ndani zaidi hadi kuwahusisha karibu maofisa wa kada zote katika mfumo wa utawala.
Wapo wakuu wa baadhi ya idara nyeti serikalini wanaotumiwa kuhakikisha uchaguzi unaibiwa na hakuna kinachofanyika kuzuia jinai hii. Wahenga walinena: Ateteaye mtuku ni tangauko la bure.
Mara nyingi unajiuliza, kwa mfano wale waliopewa uongozi wakaufuja kutokana na tamaa zao za kifisadi wana nini jipya la kulifanyia taifa? Wengine wamefikia hatua ya kuwaandaa waandishi wao wa habari kuanza kuwasafisha ingawa hawasafishiki.
Chanzo: Tanzania Daima.

17 comments:

Anonymous said...

Sifa ya kwanza wagombea cheo cha urais Tanzania na Bara lote la Afrika kwa ujumla lazima kuwa na hila za mnafiki.

Kamwe mtu sahihi mzalendo, mbunifu na makini kugombea cheo cha Urais Tanzania hawezi hata kutamka tuu nafikiria kugombea Urais.

Kimsingi hawa wote wanaojitokeza sasa wapo wainaishi katika bwawa la uwozo na pia wanafurahia kuishi katika hali hii. Hivyo wote wana uwezo wa kuona

lakini hawana maarifa ya kujitambua kutekeleza vitu kizalendo. Hawa wote na wengine hawatufahi. Kinachotakiwa hapa lazima kwanza chama hichi cha Chukua Chako Mapema(C.C.M).

Kiondolowe madarakani kwa nguvu ya wapiga kura, ili kishike adabu kwa kurandaranda mtaani kwa miaka kadhaa ili watambue kuwa wapiga kura ndiyo wenye nguvu kuliko hivyo vyao vya dhamana ya umma.

Hii ndiyo tiba pekee katika maendeleo ya Tanzania. Vingenevyo tutaendelea kuchoma mahindi.

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Anon shukrani. Umetoa somo kubwa sana. Heri wahusika wazingatie kabla hawajajirejesha kwenye mateso mengine kwa kuchagua mafisi mafisadi na vitimbakwiri ili wawaumize. Safari hii tusifanye ajizi. Tuipige chini CCM. Huu ndiyo utakuwa mwanzo wa ukombozi wa kweli.

Anonymous said...

Uwozo mwingine hupo huko ughaibuni kufungua matawi ya vyama vya siasa ambayo kimsingi yanawachanganya wapiga kura iwapo kama kuna matawi ya vyama hasa hichi kilichopo madarakani basi kwa mpiga kura tafsiri yake ni kwamba hichi chama kinaungwa hata na watanzania wanaoishi ughaibuni hivyo kitakuwa ni chama sahihi.

Kumbe ni wajinga wachache wenye fikra za kuona tuu bila kutambua wanafanya haya.Wanoafikiria kupitia tumboni kama hao wengine waliopo

Anonymous said...

Nasikia kichefuchefu na kutapika. Nikiona sura hizo eti zinataka. URAIS
Wanaiiba pesa za Tanzania. Maficho ya pesa Dubai
Kwa mgombea urais

Anonymous said...

Wanafungua matawi ughaibuni ili kuficha ufisadi na kusema tumechangiwa na Watu toka ughaibuni kumbe ni pesa zetu za kodi pls Watanzania msigauwe CCM
Mwakani
Mtamjua mengi baada ya hapo

Anonymous said...

Na wote wanachama wa CCM ughaibuni ni mafisadi au wanaishi bila Vibali ughaibuni na CCM inawabeba wengi wao ni wauza sembe ughaibuni tunajua fika

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Anon hapo juu mmesema kweli. Siyo sote tunaoishi nje tunashabikia uoza huu. Ukiangalia wanachama kwa mfano wengi wa CCM nje ima ni watoto wa vigogo au wale walioshindwa na maisha huku kiasi cha kutafuta gea ya kurejerea nyumbani kuepuka aibu ya kuishiwa. Mtu ambaye yuko ughaibuni kwa shughuli zake za maana zisizohitaji Godfather serikalini hahitaji kuwa mwanachama wa chama au kufungua matawi ya kijambazi. Matapeli ambao hata wengine si watanzania wanatumia gea hii kuwa karibu na ubalozi ili waweze ku-survive. Nadhani matawi ya Washington na London wanaongoza kwa upuuzi huu. Wachunguze wengi wa wanaojiita wakereketwa au waulize taaluma na shughuli zao. Japo si wote, wengi wa wanaoshabikia vyama wana matatizo. Ni bahati mbaya hata vyama vya upinzani vimeingia mkenge wa kufungua matawi nje. Kwa wanaokumbuka vijiwe vya CCM na jinsi vilivyokuwa vikifunguliwa na watu kuvitumia kufanya biashara chafu kama mihadarati na umachinga hata utapeli. Vimeishia wapi? Uchaguzi ukiisha vinafishwa kwani watawala wanakuwa hawana haja navyo tena na matapeli wanaovitumia wanajua hivyo. Ngoja mwakani usikie vitakavyofufuka tayari kwa matapeli wa kisiasa na kiuchumi kutumiana.
Kwa ufupi ni kwamba kinachoitwa matawi ya ughaibuni ni conduits za ufisadi mfano mafisadi kujifanya wamechangiwa na washirika wao wa nje wakati si kweli.

Anonymous said...

Hapo hakuna rais wala marais
Wenye uraisi wako pembeni wata fanya danga Kama la Spika wamchague Dr migiro alishindwa kazi UN
Hawezi kufanya kazi huyu mama Hana confidence
Hajiamini ni muoga na mafisadi watamtumia huyu Kama walivyofanya kwa Anna Makinda

Anonymous said...

Inashangaza rais wetu ana wasaidizi wake eti kwa wanganga na wanalipwa na kodi zetu
Hawa wasaizidi hawakwenda shule Ila ni Watu wanaoamini uganga

Anonymous said...

Kuna mgombea mmoja hapo mkewe ni shangingi
Mwizi kwenye mahoteli huiba taulo mpaka glass
Je akiwa First Lady ataiba vingapi
Mumewe waziri sasa

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Anon hapo juu nimewasikia. Kweli niliwahi kusikia kuwa rais ana mganga wake wa kienyeji ambaye habanduki kila alipo. Ukisikia upuuzi ndiyo huu. Kana ni kweli nani anahitaji rais mshirikina. Hili la Migiro kutojiamini nilishalisikia mara nyingi. Hata hivyo sishangai. Kama waliweza kumsimika mtu wa hovyo kama Anna Makinda kuwa spika watashindwa nini kwa Migiro? Nadhani CCM wanahitaji watu wa hovyo kama JK. Hili la waziri mwenye mke shangingi nashauri mtoboe lau wadau wamjue. Nawashukuruni kwa michango yenu adhimu wadau.

Anonymous said...

Umeyasikia ya USA uchaguzi wa viongozi tena si wa chama Bali viongozi wa Watanzania Washington
Umechakachuliwa tena na balozi Yule mama hata mwaka Hana. Na mtoto wa nyanganyi si sujui wamepokea maagizo toka bongo
Haningi Kichwani balozi. Hata mwaka Hana hawajui Watu hata Kama alifanya kazi USA lakini Watu wa mtaani balozi anawajua jamani
Hii inadhilisha vipi CCM wanavyochakachuwa kura zetu bongo
Na ninyi I Watanzania wa Washington. Si mu anzishe umoja mwingine kuwakomesha mafisadi hao

Anonymous said...

Alikuwa balozi mwanaid hatujasikia kashfa hizi
Mwanaidi njoo UKAWA ulikotoka kabla ya CCM
Tuchaguwa Kuwa urais unafaa Huna makundi na una kwenda wakati hata wazungu England na USA na dunia nzima wanakukubali
Hata bongo unamshinda migiro Kabisa

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Mwanaidi Majaar ni fisadi wa kawaida ambaye kampuni yake ya uwakili imesaidia mikataba mingi ya kifisadi. Hafai ni kwa vile hammjui vizuri mnaomtetea. Fuatilia mawakili kwenye sakata la EPA utagundua ukweli unaomuumbua huyu fisadi. Usitegemee Kikwete ateue mtu safi kwenye wadhifa mkubwa hivi hivi.

Anonymous said...

Sikujuwa yote haya

Anonymous said...

Cha msingi hakuna mwana sheria msafi
Ukiwa mteja pesa I naongea hata Kama ukiwa unamakosa wanajua kupindisha sheria that's why milimani tulikuwa tunasema digrii ya kitandani enzi za mzee kunji

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Anon hapo juu Lol! Ila kumbuka madude ya sheria ni magumu na si digrii ya kitandani kama layman anaweza kuchukulia. Hayo tuyaache. Hili la kufuata fedha kidogo linaingia akilini ila daktari anapoapa hapaswi kubagua nani mhalifu na mgonjwa wa asilia. Nadhani wanasheria wanaongozwa na sheria zaidi ya unavyoweza kudhani.