The Chant of Savant

Saturday 10 May 2014

NGO ya Bi Mkubwa haitakuwa WAMA au WA-KUSINI

 
Naingia nyumbani nikiimba wimbo wanu kipenzi. Huwa napenda kuimba wimbo huu ili kuonyesha usomi wangu usio wa kughushi wala kupendelewa.
Comment voulez vous, Que je vive, Que je parle
Que je ris, Et que vous, j’ existe, Se lui comment avant
C’est aux autres, Toujours que ca, Arrive
et voila  la ,Difference est la,Voyez je suis la
Chante, Ma vois est la meme
et je n’ai pas , Changer , Mes chansons
 Tafsiri ya kilevi
Jua ni kwa ajili yako naishi, japo wengi huja na kupita, ni wewe naimbia
Naonyesha ilipo tofauti hapo ilipo tofauti.
 
Voila la difference la, il faudra lon…, Longtemps
Et que il passé, Les temps Mais vous n’y, Croyez vou.
Hiyo ndiyo tofauti naiona tofauti.
Ilikupasa kutambua siku nyingi ila huelewi wala kuamini.
Wimbo wa Sylvie Vartan niliyesoma naye kule Paris wao huita Parie. Hayo tuyaache nisionekane kama najidai na kujipa ujiko.
Baada ya kusukuti tuliyoongea na walevi kuhusiana na Katiba mpya iliyogeuzwa mradi wa kutengeneza njuluku na mavuvuzela, naamua kujiimbia huo wimbo kipenzi huku nikisukuti jinsi ya kwenda kumkabili bi mkubwa ambaye tulikosana asubuhi kabla ya kuelekea kwenye kanywaji. Naingia kama kawa na kumwamkua japo hajibu. Nadai ugali wangu na kuula kimya kimya tayari kwenda kupiga mbonji au vipi?
Baada ya kudunda kitandani si niliota kuwa nimechaguliwa kuwa mkuu!  Hii mibangi na mma bwana, matataizo matupu! Stori yenyewe ilikuwa ifuatavyo:
          Baada ya kuupiga mma na mibangi kunibangua si nikaota eti nimechaguliwa kuwa rais wa kaya. Wacha nikurupuke usingizini na kuanza kupanga mipango ya kuwakomboa walevi. Si utani. Niliota kweli nakuwa rais wa kweli kweli na kukaa kwenye ikulu ya kweli pale Magogoni.
Baada ya kuota ndoto hii tamu, kitu cha kwanza kilichonijia akilini ilikuwa ni kumkomesha huyu bi mkubwa kidomodomo ambaye usiku ule alinishiti na kuniacha nipigwe na baridi asijue kanywaji kalikuwa kakinipa joto hata kuliko yeye.  Kwa taarifa yenu, kama alivyowahi kusema Njaa Kaya: Kelele za mpangaji hazimzuii mwenye nyumba kuuchapa usingizi.  Si vizuri kusema mambo yote ya bedroom. Hivyo, mengine nitayaruka hasa maongezi yetu na ile mijadala ya kutafuta suluhu ili lau kieleweke. Hayo tuyaache.
Baada ya kuota ndoto ya ukuu, nilipanga nimwamshe na kumpa live kuwa nikiingia kukuu aliye na kuomboleza. Maana, sitamruhusu kutumia ofisi au ujiko wangu kutengeneza njuluku kama ilivyo. Ikizingatiwa tulivyolala tukiwa tumenuniana, kwa nijuavyo domo lake, huenda angewaamsha majirani. Hivyo, niliamua kuendelea na mipango yangu bila kumsumbua.
Nilipanga kuwa nikiingia ulajini lazima bi mkubwa ausikie magazetini na kuusoma radioni. Baadaye niling’amua kuwa kumzuia bi mkubwa asifaidi maulaji yangu itakuwa noma ukiachia mbali kuwa kikwazo cha utendaji wangu. Kwanza, nilisukuti nikakuta kuwa kama ningetimiza azma hii basi ningekonda. Maana msomi wa usiku ungeota mbawa baada ya mpishi mwenyewe kunikomalia na kuniminyia ili kunikomoa na kunikomesha kwa kumnyima ulaji.
Baada ya kuwaza na kuwazua niliamua nimpe ulaji ili naye asininyime ulaji. Hivyo, nilipanga kuanzisha sera ya nipe nikupe. Sina mpango na maisha bora au bora maisha zaidi ya nipe nikupe. Namaanisha kuwa ukichapa kazi vilivyo nakupa mshahara tosha na maendeleo. Ukifanya uvivu ofisini hupati mshahara zaidi ya namba kwenye lupango.
Hivyo, kimya kimya nilianza kuidurusu na kuipiga darubini Wanawake wa wakubwa na Maulaji (WAMA) iliyoanzisha na bi mkubwa tangu Njaa Kaya alipoukwaa ulaji kimazabe baada ya kuwachafua wenzake. Niligundua kuwa NGO hii tangu kuanzishwa kwake imejikita Kusini mwa Kaya na si popote. Imejenga shule ya kisasa kule Nyamisa… malizia ambako ni Kusuni. Kila ka msaada kanakopatikana na kupigwa panga kanaelekezwa South. Hata wakati wa Fursa Sawa kwa wake za Wakubwa ilipoanzishwa baada ya Ben Tunituni Makapi kuukwaa, vimbwanga vyake viliekezwa Mushie hasa Kishumundue na Ntwara kwa jamu.
Ilibidi nisukuti kwa sana tu. Hivyo, napanga kumuamuru mke bi mkubwa kuanzisha NGO ya kaya ambayo itaitwa WAKA yaani Walevi Kayani na kama itaitwa WAMA basi kirefu chake kitakuwa Walevi na Maendeleo. Hataruhusu NGO ya kibaguzi inayotumia jinsia, eneo au itikadi kama ilivyo. Pia nitahakikisha NGO ya bi mkubwa inafanyiwa ukaguzi wa mahesabu kila mwezi ili kukwepa kuzidiwa kete na maulaji yangu yakatumika vibaya kuwaibia walevi kupitia misaada.
Wakati bi mkubwa akiendelea kuuchapa usingizi na kukoroma, mwenzake nilikuwa bize nikimpangia jinsi ya kutumia madaraka yangu wakati wa utawala wangu. Mimi si bwege wa kuruhusu bi mkubwa afanye atakavyo huku nikijua wazi ni makosa yanayoweza kunigharimu baada ya kuachia ngazi. Mie ni sawa na Mzee Mchonga. Lazima kumjengea heshima bi mkubwa wigo wa uwajibikaji na kumuepusha na vishawishi na ulevi wa madaraka. Si mlimsikia Prof Laurent Badboy wa Ivory Coast aliyeponzwa na Delila aitwaye Simone? Mie huko siende hasa usawa huu ambapo walevi wanazidi kujitambua na kujanjaruka au vipi?
Hivyo, kabla ya kuendelea kuuchapa niliazimia kuwa sitamruhusu atumie magari ya umma wala sitamruhusu ajihusishe na siasa uchwara. Pia bi mkubwa hataruhusiwa kuwa rais mdogo ima wa wanawake au wachovu. Na mwisho, sitamruhusu kuwa na misafara wala kuandamana nami kila mahali akilipwa per diem.
Alipogutuka usingizini nikajiambia: We! Koma, nitamruhusu afanye atakavyo ili nami nipewe nitakavyo toka kwake.
Huwa wengi wanajiuliza swali moja kuu: Kwanini wake wa madingi huanzisha NGO waume zao wanapoula? Da Flo Wingia nakuachia swali hili huenda siku moja utalizamia na kulichambua. Hata hivyo, kuna namna au vipi?
Mbarikiwe san asana. Salamu za leo ni kwa walevi wote niliofundisha nao maeneo ya Kinondoni akina Shombe, Mtakatifu Zakaria, Shambulla, Makakala, Keregero, Sanya na wengine.
Chanzo: Nipashe Mei 10, 2014.

No comments: