The Chant of Savant

Monday 16 December 2013

Mauaji ya Mabina yawazindue watawala wasiotaka kujifunza


Kuuawa kwa aliyekuwa mwenyekiti wa mkoa wa Mwanza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) si kitendo kizuri kwa taifa ingawa kina somo. Je kama jamii iliyozoea kukandamiza wanyonge walio wengi tunajifunza nini? Waingereza husema the writings are on the wall yaani maandiko yako ukutani kuwa tusome alama za nyakati. Nani alijua kuwa wananchi wa kawaida wangehimili vitisho vya mabaunsa na bunduki na kumtoa roho mtu aliyejifanya kiongozi wao lakini akatumia dhamana hiyo kuwaibia ardhi, mashamba, kuwatisha, kuzuia uhuru wao wa kutembea na hata kumuua mmoja wao kabla kondoo hawajaamua kumshughulikia fisi?
Nafurahi kuwa niliyotabiri kwenye kitabu changu cha SAA YA UKOMBOZI yanatimia haraka sana. Je tunao viongozi wangapi wanaotumia madaraka tuliyowapa kama silaha ya kutuibia na kutunyanyasa? Je kifo cha Mabina kinatoa picha gani kwa CCM? Je CCM itakwepa kulaumiwa kwa kuacha wakubwa zake wawanyonye na kuwadhurumu wananchi kila uchao bila kuchukua hatua?
Kwa wasiopenda dhuluma, kilichompata Mabina ni onyo kuwa wale waliodhaniwa kuwa vihongwe wa kubebeshwa kila takataka za wakubwa wameamka na lazima watajikomboa hata kama ni kwa kumwaga damu kama ilivyotokea kwa Mabina.Wale wanaodhani kuwa CCM itaendelea kutawala kwa kutegemea ujinga wa watu wa mashambani wafikiri upya.Kwa habari zaidi BONYEZA HAPA.

2 comments:

Anonymous said...

Hii inawezekana kuwa ni kisehemu tuu cha dhuluma na ujambazi unaofanywa na wenyewe dhamana waliopewa na wananchi kuwaongoza ni hatari na pia inatisha....

halafu tunamlilia Madiba mwancheni apumzike acheni kuleta hadithi hadithi zisizokuwa na tija wala mng'ao na faida katika watu makini

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Anon si kuwa hii inaweza ni sehemu tuu bali ndiyo chanzo chenyewe. Mabina ni replica ya manyang'au wanaojiita viongozi waliotamalaki kwenye chama cha mafisadi so to speak.