The Chant of Savant

Friday 6 September 2013

Taifa la mambo feki na mitumba

Hivi karibuni kumezuka uoza wa hali ya juu katika nchi yetu. Tumeshuhudia kukamatwa kwa askari wa traffic feki, wamilki feki wa sare za polisi na sasa daktari feki. Tuna mfumo feki. Tuna mawaziri na wabunge na wafanyakazi wengine wa umma feki. Tuna sera feki na hata taarifa zinazotolewa na serikali mara nyingi ni feki. Hivyo, si uzushi wala matusi kusema kuwa sasa tuna taifa la kila kitu feki kuanzia bidhaa hadi watu. Katika kitabu changu cha KWETU NI WAPI nawaita watu wetu na mambo yao vya mitumba. Uongozi mtumba unaoishi kwa kuomba omba na kula masalia, watu mitumba wanaofanyiwa umitumbamitumba na uongozi mitumba. Na sasa tuna taifa la mitumba kiakilli na kulhali. Je nani atatuokoa na janga hili?

2 comments:

Jaribu said...

Rais wetu mwenyewe ni dakta feki, I mean wa heshima.

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Nadhani yeye si feki tu bali dandizi na kihiyo awalindaye matapeli wenzake wanaoghushi. Tuzidi kumpa vipande vyake hata akinyamaza message sent.