The Chant of Savant

Tuesday 13 August 2013

Inaleta picha gani rais anapokutana na mateja huku akiwalinda wauza unga?

8E9U3986 62170
Rais Kikwete akiwa na mateja wastaafu ikulu hivi karibuni pamoja na Pili Misana na  Zakaria Hans Pope mfadhili wa kituo hicho.

Mwaka 2006 rais Jakaya Kikwete bila kulazimishwa na mtu yeyote alisema kuwa ana orodha ya wauza madawa ya kulevya nchini. Sasa ni miaka saba imepita tangu atwambie ana orodha hiyo. Wengi tunajiuliza ni kwanini imechukua muda mrefu hivyo kuwashughulikia wauza unga kama kweli ana nia au anangoja awashughulikie baada ya kustaafu? Ajabu juzi Kikwete alipodhalilishwa na Rwanda alikuwa mwepesi kuwatimua wanyarwanda waliokuwa wameishi Tanzania kwa zaidi ya miongo minne. Je Kikwete ana namna anavyonufaika na mihadarati kiasi cha siku hizi kuanza kujionyesha kama mtu anayewajali vijana kwa kukutana na mateja au kumsaidia teja Ray C. Je Kikwete anatoa picha gani kwa kuwakumbatia wauza unga huku akijifanya kuwapenda na kuwajali mateja? Je ni usanii au unafiki?

8 comments:

Jaribu said...

Kila siku ana orodha, orodha ya wauzaji madawa, majangili, wahamiaji haramu, nk. Laiti angedai ana orodha ya majuha, labda kungekuwa na breakthrough....

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

We Jaribu,
Huwa hukosi vituko. Unataka awe na orodha ya majuha wakati ujuha chini ya utawala wake ni ujanja? Hujasikia madaktari kughshi kama Nchimbi, Kalama, Mahanga, Nagu na hata yeye wa kugawiwa? Orodha ya majuha anayo kwa sana tu.

Anonymous said...

Hivi jamani, tulikosea wapi? Huyu jamaa na kikosi chake mimi nilianza kuchoka pale alipokuja na "orodha" (ambayo hata havyo hakuitaja sana) ya mapanja wa EPA n.k.miaka ile. Alinichefua aliposema eti wakichukukuliwa hatua "nchi ingeyumba"!! Aliwapa eti "msitari mfu" warejeshe walichokwapua...! Hebu thubutu kunyakua "kimobiteli" cha mtu pale mjini halafu ukishitukiwa ujifanye eti unakirejesha....thubutuuuu! Utauawa mchana kweupeee.

Mara nyingine sasa ninadhani ni bora tu nchi "ingeyumba" wakati ule, lakini watu walau wangekuwa na heshima na uoga na mali ya umma.

Leo hii tunasikia kuna baadhi wanasema kushughulika na ma-bosi wa "sembe" pale mjini ni sawa na kufanya mapinduzi mapya. Jamaa anacheka cheka tu na "mateja wastaafu" huku akifumbia macho chanzo cha mateja.

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Anon usemayo ni ya msingi. Heri nchi ingeyumba wakati ule watu wakatia adabu. Hata hivyo, kutokana na madudu ya huyu jamaa, tuendako nchi itayumba tena sana. Maana umma hautavumilia kuendelea kutenzwa kama nepi na punda huku majizi machache yenye madaraka na koo zao na waramba viatu wao wakineemeka. Umma lazima utauchoka ukupe na ukondoo na kuamua kuchukua hatua. Haya mapinduzi ya kupashana habari si mchezo. Kuna siku kibao kitageuka na watalia na kusaga meno kama siyo kuishia lupango au kumiminiwa risasi. Nani alidhani kuwa nguchiro kama Gaddafi angeuawa kama kibaka?

Anonymous said...

Anafikiri sisi tusemeje sasa fr. Mhango? Bila shaka na yeye ni teja mstaafu, maana kwa raisi mwenye akili timamu hawezi kutoa kauli kama hii '....wasichana wanaopata mimba shule za kata wana viherehere..!' Hii si ni kauli ya teja kabisa? Mimi nasema yeye ni teja na hao ni washirika wake!

Anonymous said...

Anafikiri sisi tusemeje sasa fr. Mhango? Bila shaka na yeye ni teja mstaafu, maana kwa raisi mwenye akili timamu hawezi kutoa kauli kama hii '....wasichana wanaopata mimba shule za kata wana viherehere..!' Hii si ni kauli ya teja kabisa? Mimi nasema yeye ni teja na hao ni washirika wake!

Jaribu said...

Kweli Mhango, sikujua kuwa orodha ya majuha inamaanisha baraza la mawaziri.

Anonymous, mimi zamani nilifikiri kuwa kauli za huyu Dakta Usiniamshe ni dalili ya udhaifu wa fikra, lakini theory yako ya uteja ina mvuto zaidi.

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Jaribu unategemea nini kama baraza la mawaziri limejaa vihiyo walioghushi vyeti vyao na asiwafanye kitu kwa vile ni wenzake? Kwangu hili si lolote si chochote bali orodha ya majuha wanaouza nchi yetu hata kama wengi wao wana PhD kama J4 Kawa-dog. Kusema eti wanafunzi wanaopata mimba ni kutokana na kiherehere ni ushahidi wa ujuha na kukwepa tatizo bila shaka.