The Chant of Savant

Saturday 13 July 2013

Walevi wavunja radio ugeni wa Obama


   Tulimshambulia Black Obama, jamaa aliyewapagawisha wapenda sifa hadi wakajidhalilisha. Tulimpa `kanywaji’ na kushushia na utumbo na mapafu hadi akachanganyikiwa na kusema, don’t kill me with kanywaji you boozers.
  Alitusifia ukarimu wetu na jinsi tulivyobana matumizi tofauti na walevi wa sifa, waliokufuru kwa kufuja na kumtumia Obama kuiba fedha za wachovu. Kimsingi, kinachoitwa ukarimu si ukarimu chochote, bali kuwanyonya makapuku.
  Hivi kaya kapuku inapata wapi jeuri ya kufunga shughuli za uzalishaji kama vile kufunga barabara na mitaa wakati kufanya hivyo kunaathiri uchumi wa mtu mmoja hata kaya? 
  Sisi tulimpa makaribisho kwenye baa tunakonywea. Hatakufanya marekebisho ya baa yetu kwa kuipaka rangi upya kama wao walivyafanya baa yao. Wala hatukwaambia wahusika wazibe mashimo kwenye barabara ya kuelekea kwenye baa yetu.
  Walevi si watu wakujikomba na `kujigonga gonga’ kama vyangu. Sisi tunafanya kweli kwa kukata `kalaji’.  Ukishapata `kalaji’ unafukia mashimo wala hayaonekani.
Hivyo, tulijua angeyaona mashimo wakati wa kuingia, lakini kutoka mkeka mtupu.  Na ndivyo ilivyokuwa hadi tunamfikisha kwenye Air Fosi Wani alikuwa amechangamka usiambiwe.
  Kimsingi, ni kwamba walevi tulinufaika na ujio wa Obama kuliko wale `waliojivua nguo’ bila sababu. Sisi hatubadili jina la baa yetu na kuiita Obama.
Badala yake tuliamua kumuingiza mjini na kuita baa yetu White House kuonyesha kuwa nasi ni vidume wa vidume. Pia tulimtaka tukienda Umarekanini abadili jina la White House na kuwa Uwanja wa Fisi.
  Hivyo, siku moja mkisikia White House ikiitwa Uwanja wa Fisi msishangae. Na kweli ni uwanja wa fisi aitwaye Umarekanini.
Hata wake zetu walinufaika sana na ujio wa Michele ya Obama. Badala ya kujikanyaga na kiigereza uchwara kama cha bibi yule aliyesema I am the wife of Obama of my country like your Michele, walimkaribisha kwenye vibanda vyao vya `mamantilie’ na kumfundisha kusonga ugali.
Michele ameondoka mwenye furaha baada ya kupewa elimu ya kumuandalia mumewe chakula kilichokwenda chuo. Wake zetu waliletewa pizza. Walipoionja walisikia kichefu chefu kutokana na kujaa jibini au cheese kwa lugha ya kwao.
  Hivyo, waliamua kumfunda Michele kwa kumfundisha mapishi ya kiafrika. Kati ya vyote walivyomfundisha na kumuandalia, Michele alipenda sana dagaa wa nazi na ugali na nguru wa kurumangia.
  Pamoja na wake wa walevi kuwa `apeche alolo’, hawakujidhalilisha `kumpiga mizinga’ Michele, kwa vile wanajua hana fedha bali fedha ni za taifa.
  Walifurahishwa na kauli ya Obama kuwaambia ombaomba wenye suti kuwa maendeleo yao, yataletwa na wao wenyewe na si kwa kuombaomba. Ajabu walengwa walionekana wakinua kutokana na kuwa hamnazo.
  Kwa vile mlevi mkuu nilikuwa Sauzi, nilipokwenda kumjulia hali swahiba yangu tuliyesoma chuo Diba Madiba, niliandaa simpo ceremony kama Sauzi na Senegali.
   Maana wao hawakufuja fedha za wachovu kumfurahisha tajiri wa kutupa ili awape misaada wakati wana watu na raslimali. Sikuona Jake Zuma akikenue meno kumuingiza mjini Obama ili akate pochi.
   Jamaa yangu na rafiki yangu Macky Sall alimtolea kavu kavu kuwa ushoga Senegali haramuni. Alimwambia wazi wazi mbele yangu nikiwa naona na kusikia kuwa akome na akomae.
   Na kweli Obama alituomba msamaha kukubali yaishe. Tulifunika kombe mwanaharamu akapita kwa salama salimini.
Baada ya kumkaribisha uwanja wa fisi na kumkuna, Obama alituibia siri kuwa hakufurahishwa na jinsi walevi wa sifa walivyompokea kwa israfu. Aliahidi kututumia whisky na kutukaribisha kwenye White House.
Alituahidi kuwa hatatupokea kama wezi wala kutupitisha mlango wa nyuma kama wale. Mwenzetu mmoja alitutibua aliposema eti ziara ya Obama imekwisha turejee kazini.
   Nani afanye kazi wakati Obama ameleta neema? We ngoja utawasikia wakipeana sifa za kijinga utadhani maisha yao magumu yataondoka. Bila kuacha kutumia masaburi mkatumia akili na maarifa katika kusimamia `njuluku’ na raslimali za kaya hata aje Bill Gate mtaendelea kuwa makapuku.
   Fedha mfiche Uswisi, mtegemee kuukata Uswazi. Shauri yenu utawakata. Badala ya kuishi Kanani mtaishi kama nyani juu miti. Obama ametuahidi misaada hadi tuchanganyikiwe.
Hivyo, hakuna haja ya kufanya kazi bali kufanya kazi moja tu ya kutumbua na kukuta `kalaji’ na kuzurura Ulaya. Walevi sasa wataanza kuishi kama Wamarekani kwa taarifa yenu.
   Bling bling kwa sana na mabomu na mibunduki kwa fujo. Jamaa zangu wapingaji kaa mkao kuliwa na kulipuliwa. Hayo ndiyo maendeleo maana barabara zenu zinatengenezwa na `geshi’ lenu linapinduliwa na kubakia kanyabwoya.
   Hakuna kitu kiliwaacha hoi walevi kama jinsi mzee mzima nilivyoangusha speech tena kwa kimakonde. Ilikuwa imejaa `mipwenti’ hiyo mpaka Obama akaniabia inatosha mzee.
Maana wewe si binadamu bali chuo. mimi sikufanya kama wale ambao walipoona Obamiza akijitingisha kidogo kama anacheza wao wakamwanga radhi kama hawana akili nzuri wasijue Obama alikuwa akiwasanifu.  
   Hakuna kitu tulichomkuna  Obama kama kuwezesha kumuingiza bibi yake wa Kogelo kayani, tena bila kufuata kanuni za uhamiaji. Kwa vile kaya nzima ilikuwa imelewa uobama, tulimpitisha mipakani hata bila kuwa na pasi ya kusafiria.
   Sisi walevi wajanja. Wala hatujamkaribisha Obamiza na mingoma tena yenyewe X. Hivi ukiona baba au mama zima linakata mauno wafikiri salama? Jamani huku ni kujidhalilisha na kuonyesha kuwa urithi wa mkoloni bado unatutafuna hata baada ya miaka 50.
    Hata nilipotembelea kwenye chuo kikuu cha Harvard nilikuwa watu wanaamini kuwa urithi wa mwafrika ni mingoma jambo ambalo nililipinga sana.
   Baada ya kuwatolea speech iliyokwenda chuo waliamini kuwa mimi ni mlevi na si mpuuzi wa mingoma ya kishetani. Hivi rais na ngoma wapi na wapi? Watu wanaangalia matatizo ya walevi nyinyi mnayakwepa na kujifanya mna raha za kukata mauno wakati ni njaa tupu.

Chanzo: Nipashe Jumamosi Juni 13, 2013.

2 comments:

Jaribu said...

Ulisikia wale wajinga waliokuwa wanataka kumpa Obama shahada ya heshima lakini wakadai hawakupata muda wa kutosha? Vilevile kuna wale majuha waliokuwa wanalaani watu wanaokwenda mikutano ya CHADEMA ya masaa machache, lakini bila aibu wanawaambie watu wasije mjini siku mbili.

Labda sifa moja unayoweza kuwapa hawa vihiyo ni consistency. They are consistently dumb!

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Jaribu usinichekeshe. Hwa majuha hawakujua kuwa viongozi wa nchi huru na zilizoendelea hawaingizwi mkenge na udakatari wa mbao kama malimbukeni wetu. Hata wangesali uchi na kubembeleza Marekani isingeruhusu rais wake afanyiwe usanii kama anavyofanyiwa Vasco da Gama mpenda sifa bin Juha. Tuyaache hayo.