The Chant of Savant

Saturday 29 June 2013

Walevi kukata kanywaji na Obama

  Obama beer 1
We’ve a dream. Yes we’ve a big dream of changing the kaya. We’ve a dream to meet with Black Obama and talk business and not politics. We will taaalk and taaaalk and taaaalk.  Walevi have a dream. Lazima kuongea kimombo kuonyesha usomi wetu usio wa kughushi kama akina Lukuwi na Nchimvi.
 
Baada ya kuzinyaka kuwa rais Black Obama anakuja kutembelea kaya, walevi hatutaki kuachwa nyuma.  Tunajua jamaa ni mwenzetu anapenda sana kanywaji na tufegi ingawa tuliambiwa siku hizi ameacha.  Kwa vile mkiti nilsomea kwao Hawaii na dingi wake, najua akitoka ku-surf lazima apate kanywaji kwanza. Tumemuandalia Boha, Rubisi, Gwagwa, Nkojo, Mnazi, Ulanzi, mapuya, kangara, chibuku, common na madude mengine mengi. Tumeadaa party ya kufa mtu ila msigara mkubwa hatutapiga.  Maana FBY walisema kuwa hawapatani na kitu hii. Yes we can. We indeed can realize Bongo dream of maisha bora kwa wote.
Hivyo, nasi kama walevi wa siasa, tumepanga kumpa kampani bwana ndogo Obama ili akiondoka akumbuke siku moja aje kutupa tafu akiwa nje ya White House. Ila kwenye party yetu Joji Kichaka hatakanyaga. Tutamsusa kama tulivyomsusa rais wa Uchina kutokana na kutujazia machinga. Hata huyu wa Bangla anayekuja hatutakutana naye maana ni apeche alolo anayetafuta pa kubwaga wazamiaji wake.
  Tuna mipango kamambe ya kuhakikisha huyu Jadwong anakumbuka kuwa walevi ni mali kuliko walevi wa siasa. Onyo: Hatutatumia pesa ya walevi kujilisha upepo kumuandalia partya bei mbaya. Tumepanga tumpeleke Uwanja wa Fisi ambayo tutaibadili jina iwe White House ili apate mapupu kidogo na utumbo lau ajue asili yake. Pia, hatutamtumia Obama kuibia walevi kwa kisingizio kuwa pesa yote imetumika kumkirimia. Wala hatutajikanyaga kwake bali tutampa kampani na maongezi ya kikubwa yenye kuonyesha usawa kama walevi na wapenda haki. Yes we can and indeed we should and we will.
Baada ya kukutana na Jadwong Madwong Obama lazima tumwambie kuwa we have a dream awambie ombaomba wavaa masuti waache kunyanyasa ombaomba wavaa manyang’umyang’u kama walevi. Kwa wasiokinyaka kidhuluo Jadwong maana yake ni mtu mkubwa na Madwong ni mkubwa zaidi na mwenye hadhi kama mimi na Obama na Diba Mandela. Jadwong kwa sasa tuko wachache. Kwenye kaya yetu ni mimi pekee nimebakia baada ya Mzee Mchonga bin Musa wa Burito kurejesha namba. Hayo tuyaache. Acha niwape yale tutakayompa Jadwong Madwong mwenzangu:
Mosi, tutampongeza kushinda uchaguzi bila kuchakachua wala kutoa ahadi za kijinga na kitapeli.
Pili, tutawambia fika kuwa Bongo dream imehujumiwa na wahuni na mafisadi fulani kwa kuiba njuluku na kuzipeleka Uswazi aka Uswisi huku wengine wakifunja kwenye kuzurura badala ya kukaa ofisini kutumikia walevi.
Tatu, tutamwambia Obama mambo ambayo baadhi ya wahuni wanaficha na hawataki ayajue. Kwa mfano, tutamwambia kuwa walevi wamesikinishwa kiasi cha kuishi kwa kutegemea ofa na misaada uchwara wakati wana mikono na akili. Hivyo, sisi hatutampiga bomu la njuluku bali kumshauri tufanye biashara kwa usawa na haki.
Nne, tutampa laivu kuwa lazima tufute mikataba yote ya kijambazi ya uwekezaji katika madini ya walevi.
Tano, tutawachomea wahuni wanaotishia maisha na haki za walevi kama wale waliowamuru ndata kutupiga, kututeka hata kutuua kwa vile tunachukia uovu na ujambazi wao.
Sita, tutamshauri next time awe makini. Kabla ya kuja huku Uswekeni ashauriane nasi tumpe picha halisi ya kinachoendelea ili asijikute siku moja anakula sahani moja na wezi, majambazi, wauaji, watesaji  wababaishaji hata wahuni wa kawaida kama ilivyomtokea Tommy Blair wa kwa Mother alipopiga picha na akina Mwamali Kadhaffi wa Kashafi aliyenyotolewa roho kule Libya.
Saba, tutamshauri kuwa next time asije kwa mikwara na mibunduki na mimeli.  Maana huku watu wanalipua wapingaji kama ilivyotokea kule Arusha. Pia asiwe na hofu kwa vile sisi tutampa ulinzi wa mwagwiji wa karate wanaoweza kumeza bomu na lisilipuke.
Nane, tutashauri akija kutupa tafu asitangaze ili kuepuka kuvuruga shughuli za uzalishaji mali kama vile kufunga anga, barabara, mitaa, hata kusumbua watu bila sababu ya msingi. Maana, nilipokuwa Washington sikuona mikwara kama niliyoiona huku Uswazi ambapo kujipendekeza na kujikomba hata kwenye mambo yasiyomhusu kumezidi.  Juzi wakati nikikata kanywaji alitokea ndata aliyetaka kunisachi akidhani eti nilikuwa na bomu la kumdhuru Obama asijue ni mshikaji wangu damu. Baada ya kumkunjia kama kata sita hivi za karate ndata alitoka nduki kama kibaka. Nilimkimbiza na kumkamata na kumuonya asirudie kudhani kila mtu ni fala mwenzie. Hayo tuyaache.
Pia wake zetu wamepanga kum-surprise Mchele bint Wali wa Obama kwa kumuandalia bonge la party ambapo watamshukuru kwa kutowaibia wenzao wa Umarekanini kwa kuunda NGO ya ulaji. Juzi niliwafuma wakipanga mikakati kwenye kikao chao cha maandalizi. Nilimsikia mke wangu akisema lazima wampongeze Mchele kwa kupiga kitabu na kuacha ubabaishaji wa kutumia ulaji wa mumewe. Alisema kuwa amewapa motisha wa kupiga shule na kuwafichua waume zao watakaojaribu kughushi shahada kama wale mawaziri walioghushi Ma PhD. Nimekumbuka. Pia tutamwambia apige marufuku vyuo vya uchochoroni huko Umarekanini vinavyotoa shahada feki kwa vihiyo na waharifu wetu mabingwa wa kughushi wakitumia madaraka ya walevi. Hapa lazima watu kama Bill Lukuvi, Makorongo Mahanga, Marry Nagu, Deodorant Kamala, Emmy Nchimbi na wengine watetemeke. Soma taratibu wasiinyake wakahujumu mpango wetu wa kuwachoma kwa Obama.
Turejee kwenye shinikizo letu kwa Obama, walevi tumepanga kushitaki lile genge liitwalo Coalsced Criminal Mob (CCM- usichanganye na Chama Cha Mapinduzi maana CCM zipo nyingi). Lazima tulishitaki kutokana na ujambazi na undavandava linaofanya kwa walevi hata matumizi mabaya ya ndata kutunyanyasa wakati wakiwalinda waharifu kama vile wauza unga, majambazi, mafisadi. Hili genge la kimafia limekuwa na nguvu kuliko hata serikali ingawa inaonekana kutojua lilipo na linavyofanya kazi.
Tisa, tutambana Obama azuie wazururaji kwenda kutanua majuu kwa njuluku za walevi kama walivyomfanyia yeye asiende kutanua kwenye mbuga za wanyama. Uchumi muhimu yawe! Tutasema wazi wakiomba kwenda Umarekanini awanyime viza na kuwauliza wanakwenda kufanya nini wakati wana matatizo kibao ya kutatua.
 
Kumi, nimenusa harufu ya Air Force One.  Acha niwahi uwanja wa ndege kumpokea Obama.
Welcome to the nether world of wonders such as corruption, nihilism, bootlicking, nepotism, hooliganism especially committed by Pindaboys and whatnot.
Chanzo: Nipashe Jumamosi Juni 29,2013.

2 comments:

Jaribu said...

Hey Mhango

Hilo bomu unamezaje lisilipuke? Nitonye mwenzio kwa sababu nalilia contract ya Pentagon. Utalaam huo unahitajika sana Afghanistan na kwingineko kwenye wavaa suruali za njiwa maana jamaa wamebobea katika utalaamu wa kurusha na kutega IUDs.

On a more serious side, inasikitisha kuona mafiosi wa Tanzania wanavyojipendekeza kwa Obama. Kuwakataza watu wasije mjini, kuwazuia machinga wasifanya biashara zao na kubadilisha barabara ya Ocean kuwa Obama ni ujinga mwingine uliokithiri. Halafu wakiambiwa wanafanya upumbavu wanakasirika.

Kama ulivyogusia, Obama anapita mjini Washington au kokote kwingine bila watu kuathirika. Lakini kwa kuwa poliCCM ujanja wao ni kuwalipua watu tu na kuwapiga risasi sidhani wanaweza kufikiria dhana ya kuwapa usalama viongozi wa ndani au nje bila kuathiri maisha ya wananchi wa kawaida. Marekani huku huwezi ukawaambia watu wasiende mjini kwa sababu Dr Dimwit anawasili.

Labda kwa Obama chembe ya Ujaluo alio nayo inamfanya aone aibu kumwambia Baba MwanaAsha kuwa aache kuwaibia, kuwalipua wananchi wake na kuzurura bila mpango. Dakta Mangugu hawezi kuutambua uchapa kazi hata aikshushiwa kutoka mbinguni.

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Jaribu umeniacha bila mbavu. Kumeza bomu ni simpo. Unakula bonge la ugali halafu unalimeza. Likifika tumboni ugali unalizuia kulipuka. Dk Njaa Kaya ameonyesha alivyo na njaa ya ubongo kiasi cha kutumia masaburi tu kufikiri. Laiti ungesoma makala ya jamaa mmoja aitwaye Ngurumo Tanzania Daima Jumatatu iliyopita ungeanguka kwa vicheko. Baada ya Obama kutetea ushoga aliuliza kuwa itakukwaje ambapo Tanzania inamuacha mtu anayetetea ushoga chumbani na ba Mwana Asha.
Huku kujipendekeza kutawaacha wakilia baada ya Obama kuondoka. Maana wanadhani wakifanya hivyo atawatupia mabaki ya dola lau wapate ya kuficha Uswizi wasijue Mmaarekani ni bahiri God knows.
Kubadili majina ya barabara hiyo ni asili yao. Hawana cha kumpa Obamazaidi ya utu wao.
Kimsingi Tanzania hatuna viongozi bali maajenti wa wakoloni na viranja ambao wanaweza kufanya chochote kuwaridhisha mabwana zao.