The Chant of Savant

Tuesday 16 April 2013

Mtoto wa rais wa zamani Wade akamatwa



Mamlaka nchini Senegal yanamshikilia mtoto wa rais wa zamani wa nchi hiyo Karim Abdulaye Wade kwa makosa mbali mbali yahusianayo na ufisadi, wizi wa fedha za umma na kujilimibikizia mali kinyume cha sheria. Karim ambaye anakadiriwa kuwa na utajiri wa zaidi ya dola za kimarekani bilioni moja, alikuwa akipigiwa upatu kuweza kumrithi baba yake kabla ya kushindwa kwenye uchaguzi. Karim alikuwa waziri mwandamizi kwenye serikali ya baba yake. Karim anaendelea kukanusha shutuma dhidi yake. Mchezo wa watoto wa marais kuibia nchi zao kwa mgongo wa baba zao umegeuka kuwa sehemu ya utawala wa kifisadi wa kiafrika. Kwa habari zaidi BOFYA hapa.

2 comments:

Jaribu said...

Ridhiwani upo hapo?

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Natamani asome au asomewe kama siyo kuambiwa ili ajue ukuu wa baba yake una mwisho.