The Chant of Savant

Friday 29 March 2013

Majengo mengi Tanzania ni mabomu yanayotika



Japo habari za kuporomoka kwa jengo la ghorofa 15 jijini Dar zinasikitisha, kuna somo. Kwa wafuatiliaji wa mambo na uholela wa uwekezaji nchini ajali hii ilingojewa. Kilichojulikana si ni kama itatokea bali lini itatokea. Nadhani nchi nyingi za kiafrika kwa sasa zimejiingiza kwenye ibada za wawekezaji wengi wakiwa wageni wasio waaminifu.
Niliwahi kuonya kuwa hata daraja la Kigamboni, kama litajengwa 'kitanzania', kuna siku litaua. Tumekuwa watumwa wa pesa kiasi cha kuruhusu kila upuuzi kufanyika matokeo yake yakiwa ni vifo na maafa kwa watu wasiohusika. Ingawa rais aliwahi kwenda kujionea maafa na kutoa mkono wa pole alifaa azomewe hata kutumliwa pale. Maana serikali yake ya hovyo ndilo chimbuko la maafa haya tunayoshuhudia. Wenzetu wenye akili wanazidi kunawirisha miji yao huku sisi tukiwaiga bila kufuata kanuni za mchezo. Bila kupambana na rushwa na uwekezaji wa kipumbavu tutapoteza watu wetu wengi huku viongozi wakijifanya kuwa na uchungu nao wanapokufa wakati ukweli ni kwamba ni wao wanaowachuuza.
Sipendi kuwa mtabiri ila ukweli ni kwamba majengo yanayongoja kuporomoka ni mengi tu.

No comments: