The Chant of Savant

Monday 4 February 2013

CCM inazidi kufilisika zaidi iondoeni kuepusha vurugu


Habari za kuwapo vurugu baina ya wananchama wa vyama vya CCM na CHADEMA kule Dodoma si habari njema ingawa hakuna habari nzuri. Vyombo vya habari vimeripoti kisa cha kusikitisha na kutia aibu kilichotokea baada ya wafuasi wa CCM kushusha bendera ya CHADEMA kiasi cha kuwakera wanachama na wapenzi wa CHADEMA. Uchokozi huu wa CCM ndiyo ulikuwa chanzo cha kupigana hadi kurushiana mawe huku viongozi wa ushenzi huu wakiwa ni watu wanaoitwa waheshimiwa wabunge. Je hawa ni waheshimiwa au waishiwa? Je kuwa chama tawala ni kutawala kila kitu na kila mahali hadi kuvunja sheria? Tunalaani uchovu huu wa ki-CCM chama kinachoonyesha wazi wazi kufilisika kila idara kuanzia juu hadi chini. Kwa habari zaidi GONGA HAPA.

No comments: