Wakati wa utawala mwalimu Julius Nyerere urais ulikuwa cheo cha kutisha na kuheshimika. Kila alipokwenda hasa kwenye mataifa makubwa kama Marekani, Urusi, Uingereza na Uchina alipokelewa na wakuu wa mataifa haya huku akipigiwa mizinga 21 ya heshima. Tangu alipoachia madaraka urais wa Tanzania uligeuka kuwa kama ukuwadi wa kawaida. Siku hizi rais wetu akitembelea nchi kubwa hupokelewa uani tofauti na wakati ule wa Nyerere. Ikulu yetu imegeuka kijiwe cha wafanya biashara wezi. Rais akisafiri nje ya nchi anaficha majina ya wajumbe anaoandamana nao. Je tufanyeje kurejesha hadhi ya rais wa Tanzania?