The Chant of Savant

Saturday 19 May 2012

Wakuu wa G8 hao, waalikwa makapuku wako wapi?

G8 leaders at Camp David (19 May)
Kwa wanaokumbuka jinsi rais Jakaya Kikwete alivyojisifia kualikwa kwenye mkutano wa nchi matajiri duniani G8m wanashangaa mbona haonekani akiwa nao. Ajabu pamoja na kutuma picha nyingi za ziara yake huko Marekani ulikofanyika mkutano wa walio nazo yeye haonekani hata kuwa karibu na jukwaa akipiga picha na wakubwa wa dunia! Je makapuku waliitwa kusanifiwa na kupewa maelezo jinsi ya kunyonywa zaidi wao wakitumika kama makuwadi kama kawaida yao? Nini faida ya kufuja kodi za umma kwenye mikutano ya aibu kama hii? Kama ni kuita wenye uwezo angalau kukaribia huo ukuu kama Afrika Kusini, Angola na chumi nyingine za Afrika zinazochipukia, mbona hawakualikwa? Kunani? Watawala wa kiafrika wanapaswa kuachana na tabia ya kutenzwa kama watu wa daraja la pili wakihudumiwa nyuma ya pazia kama mizimu.

3 comments:

Miss K. said...

Hivi si nilisikia "rahisi" wa Tanzania alialikwa pia kwenye hii G8?
Hivi vyombo vyetu vya habari wana nini? Ila niilisahau kuwa Mr.misifa anavyopenda kuandikwa na kusifiwa kwa ujinga.

Jaribu said...

Si unajua upeo wa Mheshimiwa Rais?

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Ilikuwa aibu maana sikuona picha hata moja akiwa na wakuu wale kiprotokali zaidi ya moja ya kutambulishwa kama mtoto wa shule. It was a big time loss so to speak.