The Chant of Savant

Monday 14 May 2012

Kwa hili nampongeza spika Makinda



Hakika kama rais Jakaya Kikwete angekuwa muwazi hivi, lawama nyingine zingepungua. Taarifa za vyombo vya habari ni kwamba spika yuko nchini Japan kwa mwaliko wa bunge la  nchi hiyo. Tofauti na Kikwete, Makinda ametaja wazi wazi wale alioandamana nao kwenye ziara yake. Rais Kikwete amekuwa akificha orodha ya watu anaoandamana nao kiasi cha kujenga hofu kuwa kuna watu wasiofaa wanaandamana naye na kulipwa kinyume na stahiki yao. Hakika huu nao ni ufisadi wa aina yake. Kikwete hasafiri kwa pesa yake bali pesa ya umma ambao unapaswa kujua idadi na aina ya watu anaoandamana nao. Tubadilike.

No comments: