The Chant of Savant

Monday 23 January 2012

Hatimaye ICC yathibitisha kesi dhidi ya vigogo wa Kenya!





Wakenya wana msemo, "kimeumana" wakimaanisha hatari au mgongano. Kwa takribani mwaka na ushei, dunia imekuwa ikishuhudia mikiki na vituko kuhisiana na na kesi dhidi ya watuhumiwa wa mauaji ya kinyama ya baada ya uchaguzi nchini Kenya mnamo mwaka 2007-2008. Sambamba na kipute hiki, kulikuwa na mikiki ya kujipanga kugombea urais wa Kenya baada ya rais Mwai Kibaki kumaliza muda wake kikatiba mwaka huu. Hili lilifanya kesi hii kuwa na mvuto zaidi hasa ikichukuliwa kuwa vigogo wawili waliothibitishiwa tuhuma yaani Uhuru Kenyatta na William Ruto walikuwa mstari wa mbele kutaka kuwania urais.
Mbali na watajwa hapo juu, kigogo mwingine aliyethibitishiwa mashtaka ni Katibu mkuu kiongozi Francis Kirimi Muthaura na mwandishi wa habari Joshua arap Sang.
Katika mashitaka hayo yaliyohusishwa watuhumiwa sita, wawili hawakukutwa na hatia baada ya upande wa mashitaka kushindwa kuthitibisha kwa ushahidi wa kutosha. Hawa ni aliyekuwa mkuu wa polisi wa zamani (PIG), Maj Gen Hussein Mohamed Ali na waziri wa zamani Henry Kosgei ambaye ni mwenyekiti wa chama cha Orange Democratic Movement cha waziri mkuu wa sasa Raila Odinga. Kwa wachambuzi wa mambo, kunusurika kwa Kosgey ni ushindi kwa Odinga ambaye anategemea kumrithi Kibaki.
Kwa habari zaidi, BONYEZA HAPA.

No comments: