The Chant of Savant

Thursday 23 June 2011

Waje wamanga wasuluhishe gogoro hili

BAADA ya mkuu kuwajia juu viongozi wa kiroho na kirafi kuwa wanajihusisha na biasharaya bwimbiwi, nao walijitutumua na kumpa saa 48 atubie vinginevyo wanamuingiza motoni, nimeona nitoe darasa.

Mbona saa 48 zimepita na waramba viatu wamezidi kuwapasha nao wakanywea? Kumbe wote wasanii siyo?

Kwanza, walikosea hata kama naye alikosea. Hawakujua kuwa anawajua kama wanavyomjua? Isitoshe, angeogopa moto upi wakati amezoea kuishi huko? Heri wangemtishia kuwa watamwingiza gizani.

Maana tangu mgao wa kiza uanze hajawahi kugawiwa lau kwa siku moja.Pia viongozi wa kiroho na kirafi walikosea. Zamani waliheshimika sana. Lakini baada ya ushehe na uaskofu kuvamiwa na matapeli huku hata wale wa kweli wakikabiliwa na madai ya kulawiti, kuzini na upuuzi mwingine, hakuna anayewaheshimu tena.

Zamani ukimuona askofu au sheihe unamheshimu.

Siku hizi wamejaa wachungaji, mashehe na maaskofu bandia, tena wa kujipachika ili washibe karibu kila kona.

Mnamkumbuka yule aliyenaswa juzi kwakutaka kubaka? Pale kaya ya jirani na shehe yuko msambweni kwa kubaka vitoto vilivyokuja kusaka ilmu akavijaza haramu badala ya ilmu.

Ama kweli dunia imegeuka tambara bovu na gunia! Zama zile usingeona mpiga ramli au mganga wa kienyeji akiitwa shehe. Usingeona muota ndoto akiitwa mchungaji au askofu.

Wala usingeona mwizi au jambazi akiingia kukuu na kuitwa rai… we koma! Lakini kwa sasa hali ikoje?

Leo tutadurusu mambo mawili yanayounganishwa na uroho na roho za udini.

Kwanza ,tutaanza na ile kali ya mkuu kuwatolea uvivu wachunaji wa kondoo na mashehe na kuwa wanajihusisha na bwimbwi. Je, amekosea?

Hawa wanaoporomosha mishule ya bei mbaya kila kona kama si wauza bwimbwi njuluku walizinyaka wapi?

Muulize yule mama mwenye jina kama Tarehe.

Wengine hawauzi bwimbwi bali roho za waumini.

Wanatoza sadaka wakisema ni kwa ajili ya Sir God kumbe zao na nyumba ndogo zao.

Wapo wanaojikomba kwa wakuu kama ilivyotokea kwa shehe na mmoja aitwaye Amiss Matakataka aliyewatishia wapingaji kuwa wafuate sheria wakati yeye hafuati sheria wala sharia bali tumbo lake.

Shehe Matakataka upo hapo? Acha nikupashe. Pia usintishe kuwa utanisomea Albadir.

Ukinisomea Albadir mie nakusomea Al-geuza. Ukisoma kwenda kulia mie nasoma kwenda juu tuone. Kumbaff.

Kama ushehena haukulipi si uuze nyanya tu badala yakujikomba kwa wenye maulaji ili wakutupie makombo.

Shehena Matakataka amenikumbushe kijeshe na kimoja Kirundi kiitwacho Amiss kaa yeye kilichokuwa kikiwachonganisha watu kwa kujificha nyuma ya joho sijue wanajua habari zake.

Kitapeli hiki cha majoho eti kilikuwa kinajificha kwenye unyema wakati tukijua fika kinatokea mitaa ya Buja.

Hakuna kilichonichanganya kama maneno ya shehena Matakataka.

Alikaririwa akisema eti lisirikali kuwaonea wapingaji kwa kuigeuza Mahaka… (we koma utafungwa!)- nyumba ndogo yake kama geshi la mandata eti ni suala la kisheria.

Tangu lini shehena la taka lililokimbia shule likajua sheria kama si utapeli?

Eti Matakataka alikuwa akiwataka walevi wasifanye vitendo vya kisiasa wakati lenyewe bila hata ya chembe ya aibu lilikuwa likifanya vitendo vya kisiasa likijificha nyuma ya joho!

Ama kweli nyani haoni nonihino Lake. Fungeni madomo yenu kama hamna la kusema badala ya kujikomba.

Sasa mnayejikomba kwake ameamua kuwatolea uvivu.

Nakumbuka mashehena wengi huja juu pale wachunaji kondoo wanapomjia juu msaniiwakidai ni udini na chachi eti inataka kutawala kaya.

Nendeni skuli mkajifunze jinsi mambo ya kisasa yanavyoendeshwa na si kupayuka bila kuwa na vipaji naelimu ya kupayuka kama mimi.

Hebu tumgeukie Mkuu wa Kaya ambaye naye amejipayukia bila kujua kuwa anachowatuhumu viongozi wake wa kiroho kimo nyumbani mwake.

Kwanza namlaani yule mbea wake aliyetoa taarifa ya kipuuzi akipindisha maneno na kuwashangaa jamaa wa majoho wakati naye anapaswa kuzusha mshangao.

Hivi kweli huyu jamaa mwenye jina la yule jamaa wa Kwachaga aliyemtandika mkoloni kasomea uandishi au kanjanja aliyepewa ulaji kwa kujuana?

Mkuu alipayuka kutokana na kuwa na tabia ya kujisemea bila kufikiri.

Unakumbuka wakati wa mchakato wa akina Richmonduli alisemaje? Alijipayukia kuwa mgao wakiza ungekuwa historia baada ya muda mfupi.

Bila kuona mbali alijipayukia na mambo yaka mgeuka hadi kiza kikiageuka kansa au ukimwi. Si hilo tu. Moto ulimwakia hadi akamtoa sadaka swahiba yake ambaye tuna ngoja kuona kitakachotokea hapo Julai 10 zitakapoyoyoma siku kenda kumi zilizotolewa katika usanii wa kujivua gamba.

Mkuu wetu Kijiweni, amekuwana tabia ya kupayuka. Nani amesahau alivyopayuka miaka ya nyuma kuwa atawapeleka kwenye nchi ya nyama choma na ulabu akaishia kuwabamiza mkenge?

Bahati mbaya amemwambukiza hata kitegemezi chake Riz-One aliyetoa mpya hivi karibuni baada ya kufichuka chafu yake kuwa angewafikisha kwa Pilato waliosambaza nepi zake ugani.

Muulize atakwenda lini zaidi ya kufyata kia.
Chanzo:Tanzania Daima Juni 22, 2011.

No comments: