The Chant of Savant

Tuesday 12 April 2011

Somo kwa First Ladies makupe



Gbagbo, mkewe Simone na mtoto wao Michael wakiwa hawaamini arobaini yao imetimu!


Simone Gbagbo aliwahi kuitisha mkutano mkubwa wa maombi na kusema:
"Shame on Sarkozy"
"shame on Ban Ki Moon"
'Shame on Obama"
"shame on Ouattara"
Sasa ni shame on her.
Shame on Simone
Shame on Gbagbo
Shame on Michael.
Simone ndiye alikuwa mshauri mkuu wa Gbagbo kiasi cha kuwa na uvumi kuwa alikuwa na kikundi cha mauaji dhidi ya maadui wa mmewe. Kimsingi, Simone alikuwa ndiye anatawala Ivory Coast baaada ya kumtawala Gbagbo kama ilivyokuwa kwa Leila Trebelsi kule Tunisia na first ladies wengine makupe barani Afrika wanaowatawala waume zao.
Tuliwahi kutoa orodha ya first ladies makupe wanaowatawala waume zao hadi kufikia kutoa kauli kana kwamba wao ni marais.

Aspect nyingine ambayo imegeuka ugonjwa wa watawala wetu ni watoto wao ambao nao hujiona marais wakati ni makupe ya kawaida.
Aibu iliyowapata Laurent na Simone ilipaswa kuwa somo kwa watawala wetu. Lakini kwa vile wengi wanafikiria kwa matumbo, hakuna lolote watakaloambua kwenye kadhia na aibu hii ya mwaka.

4 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Kuna watu na watu waonao aibu sio hawa ndugu yangu. Ila ilibidi iwe hvyo kuwa ni fundisho kwao..kaazi kwelikweli...

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Nakubaliana nawe dada Yacinta na karibu tena ugani. Najua ulifiwa kiasi cha kupotea. Ni furaha kuwa umerejea.

Anonymous said...

Ni bahati mbaya kwamba mshipa wa aibu kwa wanasiasa ulishakatwa long tyme tangu walipoingia kwenye hiyo fani, kwa huwezi kuamini hata hiyo ya Gbagbo ni watazamaji wa hizo picha ndo wanaofeel ka-aibu but kwake si ajabu shangwe tu. Kama mtu anaweza kukwapua mimali na kung'ang'ania madaraka na asione aibu sembuse kuwa nusu uchi?

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Anonymous umenena vema. Hawa watu wameishiwa ubinadamu kiasi cha kufikiri na kutenda kama hayawani yeyote. Nia pigo na aibu kwa bara letu kuwa na watawala wenye uchu kuliko hata fisi.