The Chant of Savant

Thursday 21 April 2011

Kujivua gamba kusiishie kuwa kuvuana nguo

Rais Kikwete akimnadi Edward Lowassa mtuhumiwa wa ufisadi wa Richmond na kujilimbikizia mali
Rais Kikwete akimnadi Rostam Aziz (Kagoda) mtuhumiwa wa ufisadi wa Richmond na Dowans
Rais wa nyuma ya pazia Salma Kikwete akimandi Mzee wa vijisenti mtuhumiwa wa ufisadi wa Rada na ndege ya rais
Rais Kikwete akinmadi Amos Makala aliyetimuliwa kwa kutofaa kumshauri


Ukijua kudanganya ujue na kukumbuka. Sijui kama CCM, rais Jakaya Kikwete, mkewe na wapambe wake wana kumbukumbu.Je wanakumbuka picha za madudu haya waliyotenda halafu leo wanajifanya kugeuka? Waingereza husema: show me your friends I will tell who you are au nionyeshe marafiki zako nikwambie wewe ni nani kwa tafsiri rahisi.

Kuna swali moja ambalo CCM, Kikwete na mavuvuzela wake hawawezi kujibu. Swali ni rahisi lenye muendelezo wa mengine mengi: Je tuamini lipi kati ya sifa mliziwamwagia magamba na kashfa mnazowamwagia sasa? Je hao si wenzenu tena washirika wa ndani?
Je unafiki ni upi kati ya mliyosema na mnayotenda sasa?
Je nao wakiamua kusema ya upande wao mtanusurika au ndiyo mwanzo wa kujimaliza wenyewe?
Je kati ya magamba na kichwa cha nyoka nani hatari zaidi? Je hawa watoto wa nyoka akina Januari Makamba na Nape Nnauye wanajua haya kuwa umma unajua zaidi ya wanavyojua wao?
Aliyesimama aangalie asianguke. Je hizi picha za Kikwete na rais wake wa nyuma ya pazia Salma na watuhumiwa wa ufisadi au wale waliotimuliwa kwa kutofaa watazifuta vipi? Mtavuana magamba hadi nguo na bado mtaendelea kuwa mafisadi tu.

2 comments:

malkiory said...

Wakati anatafuta kula alituambia ni watu safi, mara leo hii wanavuliwa magamba kwa kukosa uadilifu ndani ya chama. Ama kweli shukrani ya punda ni teke! Contractions zote za nini hizi au ni ukosefu wa kumbukumbu ya yaliyopita.

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Mkuu Malkiory,
Habari za siku tele? Jamaa zako wakishakula kama mainzi bila kunawa wala kusali wanasahau kiasi cha kunya humo humo. Hiki kimbembe cha Lowassa-Chenge-Rostam litawaacha uchi wote. Hakuna atakayesalimika kwa vile wote ni wachafu amini.