The Chant of Savant

Monday 7 January 2008

Kuwauwa waandishi si jibu bali balaa kwa taifa.

Vyombo vya habari vimeripoti kumwangiwa tindikali na kukatwa mapanga waandishi Saed Kubenea na Ndimara Tegambwage. Kuna kundi la manyang’au na gwagu wanawatishia maisha waandishi wote wasioridhika na ufisadi nchini mwetu. Wanataka tunyamaze ili waendelee na uchafu wao. Mtaweza kuwadhuru hao waliomo nchini. Je sisi tulio nje mtafanyaje?

Hakika wapuuzi hawa wanapoteza muda. Wanaweza kuwanyamazisha waandishi hata kuwaua. Watafanikiwa kuua mwili lakini siyo roho wala kile tunachosimamia. Edward Modlane, Steve Biko, Ernesto Che Guevarra, Mtwa Mkwawa na wengine wengi waliuawa. Lakini kile walichosimamia na kupigania hakikufa. Msumbiji, Afrika Kusini, Bolivia,Tanzania na nchi nyingine ziko huru.

Inatia kinyaa kuwa zamani mashujaa wetu waliuawa wakidai uhuru na haki ambavyo sasa vinahujumiwa na ndugu zetu wenyewe huku wakitutishia maisha! Hawa ni wabaya kuliko hata wakoloni. Maana hatukuwa nao nasaba. Serikali na CCM inabidi zilaani na kujitenga na kundi hili. Yenyewe ndiyo mtuhumiwa mkuu wa ufisadi. Maana kama ni ugomvi wa wandishi hata wananchi ni dhidi ya yeyote awe mtu binafsi,chama au kikundi cha watu anayewahujumu.

Je CCM kwa kuendelea kukaa kimya haioni kuwa inajitia kitanzi na sifa mbaya kuwa sasa imeishiwa kiasi cha kugeuka dude linalotaka kuangamiza watu wake kwa sababu ya kulikumbusha kutenda haki na kuachana na unyangau? Je hawa wanaotishia watu maisha wamekodiwa na CCM? Je hawa ni aina nyingine ya waharifu walioamua kujiajiri kwenye kutenda na kulinda jinai?

Waueni waandishi hata kuwafunga hata kuwalazimisha wakimbie nchi. Lakini mtaua wangapi? Je hilo ndiyo jibu na suluhu wanavyotaka wananchi? Je ni njia muafaka na ya kistaarabu. Umma inabidi uiambie serikali na watuhumiwa kuwa kama waandishi hata wanasiasa wanaopinga dhuluma ya serikali watauawa nao wajiandae kulipia. Maana wabaya wa waandishi wanajulikana. Ni wale wote wanaotuhumiwa kulihujumu taifa kwa kupokea rushwa, kujilimbikizia mali, kupeana vyeo kwa rushwa na kujuana, kusaini mikataba feki na upuuzi mwingine kama huo. Hakuna mtuhumiwa mwingine katika hili.

Yaani nchi yetu imekuwa ya hovyo kiasi cha kuanza kuuana kwa sababu za kulinda uoza na jinai? Hiki ndicho walichofia akina Mkwawa, Mirambo na wengine? Hiki ndicho walichopigania akina mwalimu Nyerere? Hakika hii ni aibu kwa taifa.

Leo madai ya watanzania yako wazi. Hata kunguru wanajua kuwa watanzania wanataka haki yao siyo kuiomba wala kutishwa ili manyang’au wachache na familia zao waendelee kuneemeka migongoni mwao.

Vijana wameishatoa tangazo wazi. Kinachopingwa ni zaidi ya kile anachosema wapinzani. waandishi wajumbe na watoa habari tu. Akina Kubenea wako wengi hata kama hawajitokezi kwenye majukwaa au bungeni na magazetini. Wapo mashuleni,viwandani, majeshini, mashuleni, vyuoni safarini, misikitini,makanisani,mitaani kote wamejaa.

Wanaona watu wanavyoingia siasa wakiwa maskini na kuibuka matajiri wa kupindukia huku umma ukitopea kwenye ufukara. Wanaona na wanajua. Huu ni ukweli usiopingika. Kupingana nao ni kupoteza muda na nguvu. Anajua zinapotoka "Neema" za ghafla na waneemeka wanawajua hata kwa sura na majina hata wanakoishi na wanachofanya.


Wamekuwapo muda mrefu ila wakati wa kusema ulikuwa bado. Hata akina Mpayukaji, Ansbert Ngurumo, Freddy Macha na wengine wako wengi hata kama hawaandiki kwenye magazeti wala kutangaza kwenye matelevisheni.

kwa lugha nyepesi ni kwamba vijana wamestuka wanaulizia kazi 500,000 walizoahidiwa kwenye uchaguzi siyo vibarua. Hakuna aliyewalazimisha kuahidi.

Wanapinga "wakubwa" kujilimbikizia mali na madaraka. Serikali lazima itoe ufafanuzi na mipango inayoingia akili juu ya kuwapatia vijana ajira na kupambana na wakimbizi wa kiuchumi waliojazana nchini mwetu.

Leo wanahoji kesho wanaweza kuchukua hatua.
Leo ni watazamaji. Kesho ni wachezaji.
Wanapinga uchoyo, roho mbaya, usanii, ufisadi,kujuana, ufisi, uchangudoa na ubinafsi vinavyooonekana wazi.

Wanapinga maneno matupu bila vitendo.Wameamua kuwakabili wahusika baada ya wazee kuwaangusha kwa kuridhika na mateso wanayopewa.
Wanatangaza azimio lililowazi kama maandalizi ya kujikomboa. Waandishi wanafikisha ujumbe kwa niaba ya wananchi. Wao ni sauti ya wasio na sauti-voice of voiceless. Mnawaonea bure na ukweli huwa na tabia kuu moja. Unaweza kuzimwa lakini hauuawi hata kidogo.

Kwa mtu anayejua vikundi vya mbwa koko walamba matapishi na wachokora majalala yawe ya jinai, kisiasa na ya uchafu walioivamia CCM, ni rahisi kuwabaini wanaomtishia waandishi maisha. Ni rahisi kujua wanalipwa na nani. Bahati nzuri mahabithi hawa ni woga. Si kosa lao bali ulafu, njaa na utapiamlo wa mawazo. Hawa maskini hawajui kesho wala vizazi vijavyo! Kama nyangumi, uhai wao ni matumboni mwao. Utawajua kwa kazi zao. Wamejazana magazetini wakiimba nyimbo za kuusifia ufisadi kwa vile unawalisha na kuwavisha. Hawana tofauti na vyangudoa wauzao miili yao. Heri hata ya vyangu huuza mwili siyo roho zao hata za mama zao.

Wapo wengi. Kuna wauaji. Waandishi wa habari nyemelezi wapendao kusifia uoza. Wapambe wa wakubwa na makuadi wao. Wafanyabiashara ambao Mungu wao ni pesa. Wako tayari hata kuwauza mama zao mradi wajaze matumbo. Wapo viongozi wa vyama vya kijamii wanaowasaliti watu wao. Wapo viongozi wa dini wanaoshindwa kukemea ufisadi kwa sababu nao ni mafisadi kwenye majoho yao. Wanalipa fadhila, serikali inajua wizi wao. Inawavumilia. Wanaivumilia. Lao moja.
Kuna haja ya kujiandaa kuwahami. Wanapambana nao bega kwa bega. Zamani tulikuwa tukiwacheka wakenya kwa kumalizana wao kwa wao ili kulinda ufisadi. Tuliwacheka walipouawa akina Tom Mboya, Josiah Mwangi Kariuki, Robert Auko na wengine wengi waliopinga ujambazi wa watawala.

Tuliwacheka sana. Leo na wao karibu wataanza kutuzomea watakapogundua unafiki wetu kufanya walichokuwa wakikifanya wakati wa kiza. Karne ya 21 ni ya maendeleo ya kisayansi na kisiasa kwa watu waliobahatika kuuona mwanga.

Wanaomtishia maisha Kubenea wanapata wapi jeuri? Wanadhani watanzania ni kondoo wa kushuhudia mwenzao akichinjwa? CCM na serikali yake sharti watueleze. Serikali sharti iwajibike. Ni jukumu la serikali kulinda watu na mali zao hata kama wanaipinga. Yasirudiwe ya Stan Katabaro aliyeuawa na mbweha waliouza Loliondo. Yasirudiwe ya Edward Sokoine aliyeuawa na walafi na wapendao kujilimbikizia mali ambao sasa wamebakia kuishi wa misaada ya kujikomba kwa wakubwa maana hawana bao tena.

Yasirudiwe ya Horace Kolimba aliyewapa ushauri nasaha kwa upumbavu wao wakamkolimba wakidhani watakolimba wote waliosikia alichosema. Wakati wa kushuhudia wenzetu wakiuawa na majambazi yawe ya kisiasa au kitumwa umepita.

Kwa kadri umma unavyowashangilia wapinzani kwa kufichua uchafu wa wale wanaotunafiki kuwa ni wasafi wakati wameoza iwe hivyo hivyo katika kulipiza kisasi kama mmoja wao atadhurika. Walatini walisema sauti ya wengi ni sauti ya Mungu (Vox populi vox Dei). Nani anaweza kushindana na Mungu? Wananchi tubadilike. Tusitegemee ukombozi toka kwa malaika bali sisi wenyewe. Wabaya wetu tunawajua. Tuwataarifu kuwa watakapoanza kutuua kwa risasi, mapanga, tindikali au sumu baada ya kushindwa kutumaliza kwa umaskini, ujinga, maradhi, dhuluma nasi tutajihami kwa kuwavamia popote walipo.

Wasijidanganye kuwa hatuwajui. Hawa malaika wa kifo- messangers and agents of death- wanajulikana kirahisi. Ni sawa na majambazi wa kawaida. Utawaona maisha yao yakibadilika baada ya kujiunga na kundi la wezi wetu. Kwa vile wanapenda sifa na kujikomba kwa mabwana wao, tuwaweke alama kwa kuambiana. Tusome makala zao na upuuzi wao halafu tuweke kumbukumbu. Siku likitokea la kutokea tuwatafute mmoja baada ya mwingine tuwalipizie kwa kadri walivyotenda. Huu ndiyo ukombozi.

Dhana ya amani itatoweka kama mbinu za porini zitatumika kutatua sakata zima la kashfa za ufisadi.

Kwa mtu anayejua watu wanaosingiziwa, atasema wazi kuwa wahusika kama hawalaani njama hizi hata waende wapi hawataonekana wasafi. Kwanini shutuma zao ziamshe wauaji? Je ni wao waliowakodisha?
nkwazigatsha@yahoo.com


Ifuatayo ni taarifa ya Reporters Sans Frontiers- Paris baada ya kutaarifiwa tukio hili na Nkwazi Nkuzi Mhango hapo tarehe 7 Januari, 2008

Machete and acid attack on two journalists inside their newspaper

Reporters Without Borders condemns an attack with machetes and acid on Saeed Kubenea, the publisher of the weekly Mwanahalisi, and Ndimara Tegambwage, its editor, by thugs who forced their way into the newspaper’s office in the Dar es Salaam suburb of Kinondoni on the evening of 5 January.

“This barbaric attack is especially disturbing in a country where it is not customary to use physical violence to try to silence journalists,” the press freedom organisation said. “We note that an investigation is under way and we urge the authorities to do everything possible to ensure that those responsible are identified and receive an appropriate punishment.”

Armed with machetes and acid, the assailants stormed into Mwanahalisi’s offices at around 9 p.m., ordered Kubenea and Tegambwage to lie down, gave them a severe beating, threw acid on them and dealt Tegambwage several machete blows to the head.

“They fell on us with iron bars,” Kubenea later said from a hospital bed. “They hit me about the head and threw a burning liquid in my face. My colleague, who tried to resist, was also beaten and sprayed before the assailants stole his mobile phone.” The two journalists were taken to Muhimbili National Hospital the next day.

It seems the attack was prepared with care as witness say they saw suspicious individuals hanging around outside the newspaper’s premises earlier in the evening. Kubenea said the attack was the culmination of a series of threats against him that began in mid-2007.

He said that his car was recently the target of an arson attack and that he often received telephone threats as a result of articles published in the newspaper. “I was warned that I would be killed if I did not stop meddling in people’s business,” he said.

Confirming that an investigation was under way, regional police chief Jamal Rwambow said he thought the attack was an attempt to silence journalists who had helped to uncover scandals.



No comments: