Saturday, 14 October 2017

Shambulizi dhidi ya Lissu litaigharimu serikali

            Shambulio la kishenzi dhidi ya maisha ya mbunge wa Singida Mashariki (CHADEMA) Tundu Lissu limegeuka kongwa kwenye shingo ya serikali. Hii ni kutokana na namna shambulio lilivyofanyika; na namna vyombo vya usalama vilivyolishughulika kwa kutolishughulikia. Mpaka sasa, hakuna anayejua kinachoendelea ukiachia mbali kutokuwepo kwa taarifa za kukamatwa kwa mtuhumiwa yoyote kuhusiana na kadhia hii. Kimsingi, hii inalitia taifa kwenye kona mbaya hasa tokana na kujengeka hisia kuwa mamlaka yameamua kulichukulia, ima kimzahamzaha au kutokuwa na uwezo wa kufanya lolote.
            Kutokana na ukimya uliotawala, wapo walioanza kulitumia ima kwa manufaa yao kisiasa au kwa kutaka haki itendeke. Mfano wa hivi karibuni ni kuitwa polisi kwa Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania Ponda Issa Ponda tokana na msimamo wake dhidi ya kadhia ya kushambuliwa Lissu. Hili kidogo linachanganya. Kosa analotuhumiwa kulitenda Ponda ni kutoa lugha za kichechozi. Kwanza, lugha za kichochezi maana yake ni nini? Je inawezekana kuwachochea watu wenye akili zao kufanya vurugu au kuvunja sheria bila kuwa na sababu ya kufanya hivyo?
            Pili, kwa hali inavyoendelea, serikali inaweza kujikuta pabaya hasa ikizingatiwa wapo wanaodhani kuwa haikulipa umuhimu tendo hili la jinai dhidi ya mwananchi wa Tanzania ambaye, kwa bahati mbaya, ni mwanasiasa wa upinzani ambaye anasifika kwa kuikosoa serikali jambo ambalo ni wajibu wake kisiasa kama mpinzani. Je kwanini serikali inapata kigugumizi ima kutoa maelezo yanayoingia akilini au kuwakamata watuhumiwa ambao ilishataarifiwa  kuhusiana na kumfuatilia Lissu kwa muda mrefu bila kushgulikiwa? Hali hii, inaweza kufanya wabaya wa serikali kujenga hoja kuwa ilishiriki shambulizi hili jambo ambalo, hata hivyo, halina ushahidi tokana na wahusika kuendelea kutokamatwa wala serikali kutoa maelezo yenye mashiko.  Mfano, hivi karibuni, Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP) Simon Sirro alipoulizwa nini mikakati yake ya kuwasaka na kukamata waliomshambulia Lissu alikaririwa akisema “ahsante kwa swali lakini kwa hili sina majibu kwa sababu sitaki malumbano. Sisi tupo kwa ajili ya Watanzania wote ndiyo maana nchi ipo shwari. Mimi ndiye mkuu wa Jeshi la Polisi nchini na ninawajibika kuhakikisha raia na mali zao zinakuwa salama na kwa kweli ni salama. Kwa hiyo swali lako sina jibu”  Kiakili na kwa hali ilivyo tokana na unyeti wa suala husika, jibu la Sirro, licha ya kukosa mashiko na kukwepa kutoa suluhisho, halikutegemewa toka kwa mkuu wa taasisi iliyaominiwa usalama wa watanzania wote akiwamo Lissu. Hivi kweli, kama mkuu wa polisi anaotoa majibu ya kisiasa hivi, serikali itaepuka kulaumiwa?
            Tatu, inapaswa serikali ijue kuwa Lissu licha ya kuwa mtanzania anayepaswa kulindwa na vyombo husika vinavyolipwa mishahara toka kwenye kodi ya watanzania wakiwamo wapinzani, ina jukumu la kuwalinda na kuwahakikishia usalama watanzania bila ubaguzi wowote. Mfano mdogo wa karibuni ni kuenguliwa kwa mtangulizi wa Sirro, Ernest Mangu pale aliposhindwa kuzuia mauaji ya Kibiti yaliyotikisa taifa miezi michache iliyopita.  Nadhani ndiyo maana waandishi walimuuliza Sirro juu ya hali yake kama mkuu wa taasisi hii nyeti. Na hii si mara ya kwanza kwa Sirro kutoa majibu ya kisiasa na yasiyo ya kitaalamu. Kabla ya hapo, aliwahi kukaririwa akisema “yule kijana kwenye picha ukimwona yuko vizuri tu, sasa wanaposema anapata huduma ya kisaikolojia wakati kwenye magazeti anaonekana hii inatupa changamoto.” Alikuwa akijibu swali kuhusiana na jeshi la polisi kushindwa kumhoji dereva wa Lissu ambaye yuko Nairobi akitibiwa kisaikoloji tokana na trauma aliyopata wakati wa shambulio. Ni ajabu kwa mtu ambaye si mtaalamu wa magonjwa ya akili na trauma kutoa jibu la kisasa hivi. Sirro alijuaje kuwa dereva wa Lissu hakuathirika wakati yeye si mtaalamu wa masuala ya trauma? Picha pekee haiwezi kuonyesha hali ya ndani ya mhusika. Hivyo, ni makosa kutumia mwonekano wa picha kujibu masuala yanayoendelea kwenye kichwa cha mhusika. Mbali na hili, vyombo vya habari vilimkariri Sirro akisema kuwa ni aibu kwa mwanasiasa kutaka kumfundisha kazi askari anayetambua wajibu wake. Je kazi ya mwanasiasa ni ipi hasa pale inapobainika kuwa askari hakutimiza wajibu wake yaani kuwakamata waliomshambulia Lissu au kushindwa kutoa maelezo yanayoingia akilini? Sirro alionya kuwa wanasiasa wasiwafundishe siasa askari lakini yeye akaishia kutoa majibu hayo hayo ya kisiasa.
             Wakati Sirro akituhumu familia ya Lissu kutaka kufanya suala lake kuwa la kisiasa, msemaji wa familia Alute Mghwai alimshangaa Sirro na alikaririwa akisema “sisi hatupigi siasa ndiyo sababu tumeamua kushirikiana na serikali na hatuko tayari kuona suala hili linaendeshwa kisiasa lengo letu apone na ukweli ujulikane, hali ya Lissu isitumike kufanya siasa. Tunataka utaratibu wa kawaida ufuatwe bila kuingiza siasa.” Huu si ushauri mbaya wala wa kisiasa.
            Tumalizie na suala la kukamatwa Ponda. Je kosa la Ponda ni nini hasa ikizingatiwa kuwa kisheria, kusema kuwa alitoa lugha ya kichochezi haiingii akilini bila kueleza amevunja sheria kifungu gani. Ninachoona hapa, kuna uwezekano wa suala la Lissu likatumiwa kisiasa na pande zote jambo ambalo litazidi kuiweka pabaya serikali. Maana, kuna watakaojenga dhana kuwa haiwezekani serikali yenye kila nyenzo na vyombo vya upelelezi na usalama ishindwe na genge la wahalifu wachache pasiwepo namna. Shambulizi dhidi ya Lissu litaigharimu serikali isipokuwa makini na kuwakamta wahusika huku ikiwataka watendaji wake kuacha kutoa majibu ya hovyo na ya kisiasa.
Chanzo: Tanzania Daima j'pili kesho.

Mlevi amkumbuka mzee Mchonga Nyerere


          Baba Mwl JKN Mchonga, shikamoo,
            Japo umelala kwenye pumziko la milele, naamini unaniona na kunisikia. Kama hutanisikia, wengine watanisikia.  Hivyo, sina shaka utasoma hii kitu ambayo nakuandikia wakati nikikumbuka mwaka wa 18 tangu ututoke kwa masikitiko makubwa.  Habari za huko? Je ulishaonana na akina Nelson Mandela, Sir Ketumile Masire na kijana wako John Garang de Mabior yule wa Sudan uliyemsaidia akasomea kule Lushoto? Basi baba, alifariki kwenye ajali ya kutatanisha akitokea kwa  M7. Kifo chake kilisababisha kifo cha Sudan. Kwani Sudan uliyoacha moja sasa imegawanyika kati ya Kaskazini na Kusini, Waafrika na Waarabu feki, Wakristo na Waislam bila kusahau Darfur na Nuba Mountains  ambazo nazo ziko matatani zikipanga kutengana na Sudan ya Kaskazini inayobagua waswahili wazi wazi wakati nao ni waswahili wanaoongea kimanga tu kinachowalewesha kiasi cha kujihisi wao si waswahili bali wamanga.
            Baba, je una habari yule kijana wako mwingine uliyemsaidia kule kwa Nduli Yoweri M7 bado yuko madarakani huku akiwa kwenye harakati za kubadili katiba ili aendelee kuwahenyesha walevi wa UG? Anataka kugeuka Kamuzu Banda wa kizazi hiki. Basi baba, siku hizi kubadili katiba ili kubakia madarakani imegeuka fasheni. Burundi na Rwanda walishabadili zao. Kama nilivyosema, UG ndiyo hiyo iko mbioni. Hapa kwetu bado. Wapo wapuuzi fulani walifikia hata kupeleka mswaada Mjengoni wakitaka ukomo wa urahis uondolewe.  Baba, tena kabla sijasahau, una habari kuwa kwa sasa tuna rahis mpya aitwaye Joni Kanywaji Magu? Kijana huyu ni madhubuti sana pamoja na udhaifu kidogo. Kwani, tangu aingie pale Patakatifu pa Patakatifu, ameanza kuisafisha kaya kiasi cha mafisadi mapapa kuanza kunonihino kwenye debe.  Kijana amerejesha heshima ya kaya si haba. Kwani ninapokuandikia, Muhimbili kuna vitanda vya kutosha. Shule zote za Msingi zina madawati. Jamaa amebana matumizi.  Hataki kuzurura kama yale mabalaa mawili moja ulilopiga tafu na jingine ulilopiga chini  yalivyokuwa yakizurura huku yakiongozana na misururu ya walaji.
            Tena kabla ya kusahau, mama Maria siku hizi anazeeka kiasi cha kushindwa kuhudhuria baadhi ya sherehe. Hata hivyo, bado wamo si haba pamoja na umri kushuhudia. Naona unatikisa kichwa. Usifanye wivu hasa ikizingatiwa kuwa huyu ni bibi yangu. Hayo ya wajukuu tuyaache.
            Mwalimu, sasa niruhusu kwa heshima nikupe salama za walevi wako wa justice. Wanakumiss ile mbaya. Hakuna siku inayopita bila kukumbuka. Mwalimu, huwezi kuamini kuwa umaarufu wako unapanda kwa kasi kiasi cha kuwapita wengi wa walio hai hasa wale waliobomoa mema yako yote uliyoanzisha tokana na ima ubinafsi, ujinga au upogo. Hapa ninapoandika, wengine wanalindwa na kifua cha munene. Vinginevyo, wangekuwa wakinonihino kule Keko kama siyo Segerea.
            Mwalimu, good news ni kwamba yale madini uliyokuwa umegoma kuchimba wakaja wakora wakayachimba na kuyagawa kama peremende sasa yanaanza kuwafaa walevi. Haka ka kijana ka Joni kameamua kufumua mikataba yote ya kipuuzi ili lau walevi tunufaike na mawe yetu kama ulivyoona mbali. Basi Mwalimu, baada ya kajamaa kutia timu ikulu si kalianzisha mchakato wa kufumua mikataba yote. Wengi wa waliofanya upuuzi huu wanaishi tumbo moto wasijue nini kitawatokea kesho yake.
            Je unakumbuka ile kashfa ya IpTL? Yule nshomile na gabacholi waliojiona kuwa serikali ndani ya serikali sasa wanaozea korokoroni baada ya Ka-Joni kuamua wapewe haki yao. Siku hizi kuna heshima kama zama za utawala wako. Mafisadi hawatukogi kama ilivyokuwa baadaye.
             Mwalimu, unaweza kuamini kuwa siku hizi kugeuza ofisi za umma nyenzo ya kuombea rushwa na kupiga domo ni historia?  Mambo yamebadilika. Hata wale walioghushi sifa za kitaaluma, japo si wote kutokana na baadhi wachache kukikingiwa kifua, wanalia na kusaga meno. Hata hivyo, zoezi hili lilikufa ghafla baada ya kitoto kimoja chenye kujikomba kwa munene kubainika kilighushi vyeti, hivyo, kufanya akikingie kifua na kuamua kuachana na kuwasaka vilaza na vihiyo wengine.
            Mwalimu, miaka 18 si haba. Tangu uondoke mambo mengi yametokea mojawapo ikiwa ni kutimia kwa ndoto yako ya kuhamia Dodoma. Ninapoandika, wizara karibia zote zishahamia huko. Ngoja, nilitaka kusahau. Una habari kuwa siku hizi Dar  na Mwanza zina flyovers zile tulizokuwa tukizisikia Nairobi? To make things worse, kuna daraja la kuunganisha Feri na Kigamboni na linaitwa Nyerere.
            Kwa vile mhariri amenipa nafasi finyo, naomba Mwalimu niachie hapa kwa machache toka mjini niliyokujulisha. Muhimu, tunakupenda; tunakukumbuka na kukumisi kichizi na kinomi mwalimu.  Kwa leo ni hayo. Basi piga mbonji peponi milele mwalimu.
Chanzo; Nipashe J'mosi leo.

Wednesday, 11 October 2017

Reflecting on the legacy of Mwalimu Julius Nyerere

Image result for nyerere's photos
October 14, 1999, Tanzania lost its founder the late Mwl Julius Kambarage Nyerere at Guy’s and St. Thomas Hospital in London. Now, it is 18 years since Mwalimu or teacher as ,he’s famously known, sadly and untimely passed on. In pondering on Mwalimu’s legacies, as we celebrate his exemplary and unique life, it is better to wholeheartedly and thankfully bring him back to our memories and prayers. The crème de la crème per se, small man with a big heart; and, above all, unparalleled virtuous man; yet a mountain-like leader, no doubt; Nyerere contributed superbly and enormously to Tanzania and Africa in general. Due to such unrivaled makings, sans doute, his persona and stature have glowingly been growing exponentially as they days go by so as to outpower some living leaders. His shoes, too, have grown so big that nobody can slink and fit in. This is Nyerere I commemorate. I must admit from the outset. It is not easy and possible to enumerate Nyerere’s good deeds as opposed to his shortfalls despite their good intent.
            In commemorating Mwalimu, I’d like to revisit his shinning heirlooms though in a nutshell.  Who’s Mwalimu Nyerere? He’s Tanzania’s first honest and selfless president who truthfully and practically said what he did and did what he said.  Despite ruling Tanzania for 24 years, Nyrere left no hanging cloud over his people. He died a pauper by today’s standard when presidency is a very money-spinning business that makes freebooters, their families, friends and hangers-on filthly rich. For Mwalimu, nothing was important like seeing Africa being liberated from the fangs and pangs of colonialism, injustice and all criminality that made it stroppy in all spheres of life. Practically, Mwalimu fought for the dream of an independent Africa. His was to see Africa being freed from diseases, ignorance, injustices and poverty which he vehemently fought.
            Secondly, Nyerere wanted a united Africa. He tirelessly tried to actualise and realise this dream to no avail thanks to his bit-by-bit approach as opposed to his counterpart Dr. Kwame Nkrumah Ghana’s founder who desired and worked for a single-stroke one. However, despite his fiasco in actualising his dream for Africa, he left us with a token in the Union between Tanganyika and Zanzibar that gave birth to the current United Republic of Tanzania (URT) the only existing and exemplary union in Africa.
            Thirdly, Mwalimu fought and established an egatalirian society that did not have evils such as tribalism, greed, and holier than thou. He established Ujamaa na Kujitegemea or African Socialism and Self-reliance. Under his rule, Tanzania was a shining star thanks to his probity, intellect and insight. As a leader, Nyerere introduced free social services to his citizen in order to make sure that they all moved equally and together which Tanzania lost after Nyerere willingly relinquishing power in 1985 after Mwalimu admitted that his policies had failed. Again, did his policies fail? Not at all; they were sabotaged by internal and external capitalistic and imperialistic enemies who didn’t get an opportunity bully and exploit Tanzania as they deemed fit back then under Nyerere's watch.  Many Tanzanians, particularly his party the Chama Cha Mapinduzi (CCM) beseeched him to soldier on; but he told them that he was not ready to turn back and become a biblical pillar of salt to which the wife of Lot, Ado or Esther, turned into after turning back contrary to God’s instructions as they escaped from a wicked Sodom.
            Before retiring, Nyerere admonished Tanzanians to pull together. However, soon thereafter, things changed dramatically and negatively. Slowly, the lust for illicit wealth became a norm. The story is very long. For, three regimes that followed after Mwalimu’s corrupted and destroyed almost everything Nyerere stood and lived for. Some of his successors started to illicitly accumulate wealth so as to make the gap between the haves and the have-nots to grow exponentially. It reached a point at which many Tanzania wished Nyerere would have soldiered on. Corruption became legalised through the back door while ethics was replaced with ineptitude, greed and venality.  However, if Nyerere were to raise from the dead today, at least, he would be happy due to the arrival of the current president John Pombe Magufuli who seems to readjust Tanzania back to the right direction shall he stay the course.
            Nyerere’s flipside
            Nyerere was referred to as a benevolent dictator under whose rule democracy was stifled. So, too, Nyerere has a role in some of the noes that transpired after vacating from office. One of them is his superimposition of his handpicked candidate in the 1995 general elections who ended up betraying him and his cause. Notably, Nyerere saved the country from one evil to end up settling on another. Apart from that, Nyerere’s name will always be embossed in gold as far as the history of the liberation of Tanzania and Africa is concerned. RIP Julius Kambarage Nyerere Burito a true son of Africa. Amen.
Source: Citizen Wed., today.

Tuesday, 10 October 2017

Tunapoadhimisha miaka 18 ya kifo cha Mwl Nyerere

Image result for photos of julius nyerere
            Wiki hii ni ya kuadhimsha miaka 18 tangu baba wa taifa Mwl Julius Kambarage Nyerere atutoke hapo tarehe 14 Oktoba, 1999 huko mjini London Uingereza. Kwa wale waliozaliwa kipindi hicho, sasa ni watu wazima wanaoweza kupiga kura na kufanya baadhi ya mambo kama watu wazima kwa mujibu wa sheria.
            Watanzania wengi wenye miaka kuanzia 35 wanamkumbuka Mwalimu Nyerere kama nguli wa siasa aliyotoa mchango mkubwa si kwa Tanzania tu bali Afrika yote. Kiongozi mwenye maadili na asiye na makuu wala ubinafsi, mwalimu Nyerere anaingia kwenye vitabu vya historia kama kiongozi aliyejua alichokuwa akifanya hasa yanapokuja masuala ya uadilifu, uwajibikaji, usawa, na haki kati ya mengi. Kwani aliyahubiri haya na kuyaishi tofauti na wasanii wengine wanaotumia siasa kama nafasi ya kujitajirisha. Katika makala hii ya kumbukumbu ya Mwl Nyerere nitajikita kwenye sifa binafsi kama kiongozi. Sitaingia kwenye mambo aliyofanya. Kwani, nafasi haiwezi kutosha.
            Mosi, kama baba, mume na kiongozi wa familia, mwalimu Nyerere aliwalea watoto wake na taifa katika maadili aliyohimiza. Hadi sasa, hakuna mtoto wa Nyerere tajiri, au mwanasiasa aliyepata mafanikio au nafasi ya kisiasa tokana na jina la baba yake au kusukiwa na baba yake kama wengi waliotamalaki kwa sasa iwe kwenye ubunge, ubalozi, uwaziri, na vyeo vingine kwa sababu baba zao walikuwa wakubwa.
            Pili, kama mwanaume na mume, Nyerere aliishi na kuondoka bila doa lolote la ufuska ambapo baadhi ya viongozi hutumia madaraka kujipatia rushwa za kimapenzi huku wakitoa zawadi za vyeo kwa nyumba zao ndogo. Hili linajidhihirisha kwenye uteuzi wake ambao mara nyingi haukulalamikiwa na yeyote kutokana na kujiepusha na ukabila, urafiki, ukaribu au ulipaji fadhila. Kila mwalimu alipomteua mteule wake, alihakikisha anachujwa na historia yake inawekwa wazi kupitia vyombo vya habari. Ni bahati mbaya; siku hizi uadilifu umetoweka. Kwani, si ajabu kusikia fulani kateuliwa kwenye nafasi fulani ya umma bila kusikia wala wahusika kuwa tayari kuweka wazi historia ya mhusika.  Tulifikia mahali hata viongozi wakawa wanasafiri kwa fedha ya umma na watu wasiojulikana majina yao baada ya kuanzisha mtindo wa kuyaficha. Matokeo yake, sasa tunao wateule wenye mabaka kuanzia walioghushi au kutumia vyeti vya wengine huku wakizidi kulindwa na kusifiwa wakati na wahalifu wasio na maadili.
            Tatu, mwalimu Nyerere alikufa maskini ikilinganishwa na viongozi wa wakati ule hata wa sasa ambao kwao siasa na mtaji wa kujitajirisha wao, wake, watoto, warambaviatu wao na marafiki zao. Kwa Nyerere, hili halikuingia akilini. Aliishi na kufanana na wale aliowaongoza huku akipambana kuhakikisha pengo kati ya walio nacho na wasio nacho linazibika. Kwa tunaokumbuka kijumba chake cha Butiama, tunafahamu namna alivyojengewa nyumba yake ya pili ambayo hata hivyo, alilazimika kuipokea na hukuishi mle hata kwa mwaka.
            Nne, Nyerere alikuwa muadilifu wa kupigiwa mfano. Hakuendekeza urafiki wala kujuana. Hata pale marafiki zake walipopatikana na hatia ya kukiuka maadili, alikuwa mkali kama pili pili. Rejea alivyoamuru kuchapwa bakora rafiki yake na waziri wake marehemu Abdallah Fundikira pale alipobainika kuwa alikuwa amepokea rushwa. Hata baada ya kumpa adhabu hii, Mwalimu aliwatangazia watanzania bila kujali ni aibu gani angepata muathirika. Kimsingi, alitaka huu uwe mfano na onyo kwa watanzania.
            Tano, Nyerere alikuwa msomi aliyeelimika na wa kupigiwa mfano. Licha ya kusoma hadi kuwa na shahada ya uzamili, alijisomea sana, kuandika na kuelimisha kila alipopata nafasi. Ni nadra sana kuona kazi zenye kuingia akilini za kitaaluma na kisera za wale waliomfuatia. Kimsingi, Nyerere alikuwa mtu aliyekombolewa na elimu kiasi cha kutaka iwakomboe na wengine. Ndiyo maana, baada ya kupata uhuru, aliamua kutoa elimu, afya na huduma nyingine kwa watanzania wote kwa usawa akitumia vizuri kodi zao.
            Sita, Mwalimu Nyerere alipenda sana haki na usawa kiasi cha kutotaka kutendewa tofauti na wale aliowaongoza. Mbali na kutoruhusu watoto na mke wake watumie cheo chake kujineemesha kwa njia yoyote, mwalimu aliwasomesha watoto wake nyumbani sawa na watanzania maskini aliowaongoza tofauti na waliomfuatia ambao walisifika kwa kusomesha watoto wao nje ukiondoa rais John Magufuli ambaye, kwa kiasi fulani, amefuata mfano wa Nyerere kwa kutoruhusu mkewe kuibia au kuutumia umma kwa kuwa na Asasi Isiyo ya Kiserikali au NGO ambayo baadhi ya wake waliomfuata walitumia kujitengenezea utajiri na umaarufu bila stahiki kutokana na kuwa na  kulala kitanda kimoja na rais.
            Saba, mwalimu Nyerere hakuwa muongo wala msanii. Alisema ukweli hata kama ulikuwa ukiudhi. Rejea alivyowaambia ukweli wakati akitangaza vita ya kumg’oa nduli Idi Amin imla na muuaji wa zamani wa Uganda kuwa vita hii ingeumiza uchumi wa Tanzania kiasi cha wananchi kuwa na maisha magumu kama ilivyokuja kutokea.
            Mwisho, Nyerere alikuwa mzalendo wa kupigiwa mfano. Aliheshimika na anaendelea kuheshimika kutokana na sifa hii. Si utani. Leo ukiweka jina la Nyerere kwenye kura, atawashinda wengi walio hai kutokana na sifa chache kati ya nyingi, nilizotaja hapo juu.
            Kwa ufupi, huyu ndiyo Mwl Julius Nyerere, kiongozi mahiri na mtaua ambaye ni wachache wanaoweza kuwa kwenye daraja lake duniani. Mungu ilaze pema roho ya mpendwa na baba yetu Mwl. Julius Kambarage Nyerere.
Chanzo: Tanzania Daima J'tano kesho.

Kijiwe chaadhimisha miaka 18 ya kifo cha mzee Mchonga

            Image result for the cartoons of julius nyerere    Mgoshi Machungi anaingia akiwa ameshikilia kitabu cha Ujamaa na Kujitegemea kilichoandikwa na mzee Mchonga mwenyewe. Kila mtu anashangaa. Kwani, licha ya kutoonyesha usomi, Mgoshi, hajawahi kuja na hata kipande cha gazeti kijiweni. Kila mtu anashangaa kugundua kuwa kumbe Mgoshi ni bonge la mbukuzi tena mwenye maktaba yake iliyosheheni vitabu bab kubwa!
            Kama vile amesoma mawazo yetu, Mgoshi anajisifia. “najua wengi minashangaa kuona Mgoshi nimebeba tabu kubwa tena la msomi mkubwa kama mzee Mchongameno mwana wa Musa. Msikonde. Siyo azima tiseme kia tinachofanya. Cha mno nataka tikae kama kamati ya kijiwe na kumduusu huyu ngui japo tionyeshe, heshima, kumbukumbu na mapenzi yetu kwake. Au shiyo?”
            Msomi anayeoonyesha kufurahia kitendo cha Mgoshi anaamua kula mic “Mgoshi leo umenifurahisha kweli kweli. Huyu nguli na msomi mwenzetu namkubali. Nimesoma karibu maandishi yake yote. Huyu bwana hakuwa kiumbe wa ulimwengu huu; na alikuja kabla ya wakati wake. Umenikumbusha mbali sana. Umenirudisha kwenye zama ambapo usomi ulikuwa mali na si ufisadi, wizi, na uuzaji bwibwi kama ilivyokuja kuwa baada ya mzee Mchonga kutundika daruga. Zama zile uongozi hakukuwa utawala bali uongozi. Kiongozi alifanana wale aliowaongoza bila kujali kama wanakubaliana na mawazo yake au la.”
            Kabla ya kuendelea Kanji anakula mic “hata mimi iko penda na hesimu sana hii giji hata kama nataifisa mali nyingi ya hindi. Hii zee iko tofauti. Iko sawa na Gandhi. Iko nafanya mambo kubakuba sana kwa taifani hii.”
            Kabla ya kuendelea, Mijjinga anamkwapua Kanji mic na kuzoza “Kanji, huwezi kumlinganisha mzee Mchonga na Gandhi aliyesifika kwa ubaguzi. Mlinganishe na Nelson Lolihlahla Madiba Mandela Dalibunga, Osegafyo Kwame Nwia Kofi Nkrumah, Seretse Goitsebeng Maphiri Khama, Ernesto che Guevara na magwiji wengine lakini siyo na mbaguzi aliyewabuga waafrika tena nchini mwao kule Afrika Kusini akidai kupewa haki ya kuwa tofauti na waafrika aliwaita makafiri.”
            Kabla ya kuendelea Mchunguliaji anachomekea “Du Mijjinga kumbe wewe ni tabu la historia! Unawataja majina utadhani wadogo zako! Ama kweli kusoma ukaelimika raha!”
            Kapende naye anaamua kutia guu “nakubaliana nawe Mijjinga. Mzee Mchonga hawezi kulinganishwa na Gandhi. Kufanya hivyo, ni kumdhalilisha hasa ikizingatiwa kuwa hakuwa mbaguzi wala msanii. Anyway, hayo tuyaache. Mie ningependa kumkumbuka na kumdurusu mzee Mchonga kama kiongozi ambaye hakuwa mwoga wala mbabaishaji. Alipenda sana kukosolewa ilmradi anayefanya hivyo awe na hoja nzito na zenye mashiko. Akitokea mtu wa namna hii mzee Mchonga alizoea kumjibu kwa hoja nzito na zenye mashiko. Nadhani watu kama totoTundu Lissu wangekuwapo wakati wa mzee Mchonga wala wasingechukiwa wala kumiminiwa shaba.  Kitu muhimu kilichofanya nimgwaye mzee Mchonga ni kupenda haki na usawa. Yeye hakuwa na rafiki zaidi ya wabongo. Hakuwa tayari kumkingia kifua mhalifu yoyote kama ilivyokuja kutokea baada ya kuachia madaraka. Unadhani huu ungekuwa wakati wa mzee Mchongo mizigo kama Bashit na wababaishaji kama yule mchunaji Gwajimmy wangepata muda wa kutanua na kutanuliana wakati wote wana madoa? Thubutu!”
            “usinikumbushe huyu baba ambaye aliheshimu kila mtu. Bila yeye wala mimi nisingepata hii elimu, hata  kama ni haba, niliyo nayo. Bila yeye baba na mama yangu wasingejua kusoma na kuandika. Nani mara hii kasahau elimu ya watu wazima aka ngumbaru? Mungu iweke peponi roho ya baba yetu mzee Musa Mchonga Nyerere.” Anasema Sofia Lion aka Kanungaembe. Hata hivyo anashindwa kuendelea kuongea tokana na uchungu kiasi cha kumwaga chozi huku Mbwamwitu akimfariji kwa kumkumbatia.
            Msomi anamchomekea Sofia “dada usinikumbushe nguli huyu. Maana bila yeye hata mimi nisingeweza kupata PhD zote hizi nilizo nazo. Ni nani mtoto wa kapuku kama mimi angeweza kuitwa daktari kama mimi? Ni bahati mbaya. Wengi wa walionufaika na sera na upendo wa nguli huyu wamesahau kila kitu kiasi cha wao kugeuka mafisadi papa kama akina mzee wa Vijisenti, Anae Kajuamlo, Ben Tunituni Makapa na wengine wengi. Inauma na kusikitisha sina mfano.”
            Mpemba anamchomekea Msomi “ami usemacho cha kweli ati. Kwani bila huyu nguli nani angeongelea muungano wa Bara na Visiwani? Wallahi wengine tungekuwa twaendelea kuonekana wageni kwenye nchi yetu kama si huyu maalim Nyerere.”
            Mipawa aliyechelewa kufika, hivyo, akaamua kuisoma mada kwanza anaamua kutoa mchango wake “kusema ukweli, Daganyika haitakaa ipata gwiji kama huyu tena. Maana madini kama haya hutokea mara moja maishani. Hata hivyo, napenda nitofautiane nanyi kidogo kuhusiana na gwiji huyu. Alifanya mambo mengi isipokuwa baya moja; yaani kuwaamini na kuwapigia hata kampeni mafisi walioiuza kaya yetu kiasi cha dokta Kanywaji sasa kuhangaika kuinyosha. Maana kama siyo huruma yake, huenda kaya yetu ingepata kiongozi mahiri na kusonga mbele badala ya kurudishwa nyuma.”
            Kabla ya kuendelea mzee Maneno anakula mic “ni kweli aliwaamini mafisi. Je alifanya hivyo kwa nia mbaya au kutoelewa? Tumuache mzee wetu apumzike huku tukisamehe lolote alilotenda ambalo hatukulipenda. Hata hivyo, yeye alikuwa binadamu si malaika. Muhimu tuenzi mema yake yote kama vile kutominya wale aliotofautiana nao mawazo.”
            Kijiwe kikiwa kinanoga si tukaamua twende Butiama kwenda kumpa tafu mama yetu Maria!
Chanzo: Tanzania Daima J'tano kesho.

Saturday, 7 October 2017

Mlevi atamani Tunduni angekuwa mgeshi

Rais Magufuli pamoja na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo (kushoto) na Brigedia Jenerali Dkt. Paul Massawe Meja Jenerali Mstaafu Vicent Mritaba akielezea alivyoshambuliwa kwa risasi mkononi, tumboni na mguuni  wilaya ya Kinondoni jijini Dar es salaam.
            Katika kutafakari namna kaya na wanene wake especially munene mwenyewe walivyoitikia baada ya Tunduni Liisu kumininiwa shaba na wakora wanaojifanya hawajulikani wakati wanajulikana, anatamani angekuwa mgeshi. Rejea namna munene alivyojihimu na kujilawa pale mgeshi mstaafu alivyopiga shaba. Huenda huyu Tunduni angelipata top priority kama ilivyotokea kwa mgeshi husika. hata hivyo, mlevi haelewi namna mgeshi anavyoweza kuwa muhimu kuliko muishiwa. Kama angekuwa ndata, ndata wenzake wangeliwanyaka wale waliomfanyia kitu mbaya. Na kama angekuwa munene, wote wangemwabudia na kumuogopa hata kama ni kinafiki na kwa woga.
            Tangu amiminiwe shaba Tunduni, sijasikia chama twawala kikifanya mandingo lau kutuma ujumbe rasmi kwenda Nairoberry kumujulia hali. Duh inatisha. Twapelekeshwa wapi ambapo sihasa inageuka uhasama wa kufanya mlevi. Sichokonoi wala kumchokoza yeyote, namna wanene walivyoshughulikia suala la kumiminiwa shaba Tunduni, licha ya kuwa aibu na so, inaonyesha kuna namna. Hivi kweli Tunduni angekuwa mhishimiwa wa twawala wangekaa kimya hivi? Wameshindwa hata kutoa tamko hata kwenye vyombo vya umbea! Nani hataonja mauti huyu nimsujudie?
Sasa nasema; kul nafsin zalikatu mauti yaani kila nafsi itaonja mauti. Kama wababe kama Farao aka Filauni na Nabukadnezza walionja mauti, nani atasalia zaidi ya kujilisha pepo tokana na ujuha na usahaulifu? Kama Nelson Mandela, Mzee Mchonga na wengine walipotea, nani huyu mjanja na shujaa atabakia? Shame on them all! Sijui walevi wanapelekeshwa na kupelekwa wapi iwapo wanaanza kuhukumiana na kujaliana au kutojaliana tokana na imani zao za kisiasa? Inatisha na kuhuzunisha; sina mfano.
            Sisemi kutokana na kanywaji au tujani bali ukweli mtupu au ulio uchi, naked truth. Tumefika na kufikishwa pabaya. Yaani mhishimiwa mzima anamiminiwa shaba na washenzi waliofanya hivi hawashikwi! Yethu! Laillah illa Allah! Ni sheitwan gani ametuingilia hivi kiasi cha kukosa mwelekeo huruma na utu! Japo najisemea, naamini wapo wengi wanaoshangaa kiasi cha kuhoji na kujisemea kama mimi hata kama si walevi wa kanywaji.
            Namuona Tunduni kama mdogo wangu, ndugu yangu, mbongo mwenzangu na binadamu mwenzangu anayepaswa kuhurumiwa sawa nami au yeyote yakimkuta kuhusisha hata hawa wauaji na washenzi waliotaka kumnyotoa roho bila sababu zaidi ya woga na upumbavu wao. Najitahidi kuvaa viatu vya Tunduni nimdeku mkewe na watoto na ndugu na mashabiki wake ukiachia mbali wenzake. Simdeku Tunduni sawa na nguruwe waliomuumiza. Namuona kama mwanaume, baba, mwana, raia, binadamu na asiye na hatia kama mimi na wewe na wao. Namuona Tunduni kama ninavyojiona na kukuona wewe.  Laiti wengi–hasa wale waliotaka afe–wangevaa viatu vyangu na vyake na kuondoa upumbavu wao, naamini unyama aliofanyiwa usingetokea.
            Hivi Tunduni angekuwa ndata, kweli nguruwe na wanaharamu waliomshambulia wangekuwa bado uraiani wakifaidi malipo ya jinai yao? Hata hivyo, sitakata tamaa. Kwani, malipo ni hapa hapa duniani. Laiti binadamu angejaliwa kujua yanayomgoja–sina shaka–wahalifu waliomfanyia kitu mbaya Tunduni wangelia na kusaga meno na kuchelea kutenda unyama waliotenda tokana na upumbavu na upofu na upogo wao. Hwa waliommimia shaba Tunduni wangekuwa wanaume kama si watoto si riziki, wasingetenda unyama waliotenda. Hata nguruwe–pamoja na uchafu na udogo wa ubongo wake–asingeweza kutenda upumbavu na unyama huu.
            Natamani Tunduni angekuwa mgeshi au ndata. Huenda wanene wangemuabudia na kumuogopa kiasi cha kujigonga kwake; na si kumtelekeza kama ilivyo. Inashangaza na kutisha. Kama walevi hawa wameshindwa kwenda Nairoberry hapa jirani kumjulia hali, angekuwa ugabacholini au utashani wangefanya nini? Huenda wangemtumia kwenda kufanya matanuzi kwa kisingizio cha kwenda kumjulia hali wakati wengi wanaomba anyotoke roho kana kwamba wao wataishi milele. Wako wapi akina nduli Amin, Gaddafi, Hitler na Mussolini? Wako wapi akina Osami bin Ladin na Mura Umar? Wako wapi akina Augustine Pinochet?  Wako wapi akina baby na papa Duvallier? Wako wapi akina Samuel Kanyon Doe? Nambie. Wako wapi akina Botha the Croc? Wako wapi akina Pol Pot wa Kampuchea na mahabithi wengine wengi waliofanya unyama usiomithalika? Binadamu ni nini zaidi ya kuwa manii na matope?
            Leo naongea kifalsafa ya kilevi kama mzee Mchonga na Mandela kama si Nkrumah na Lumumba. Wamanga husema: pen is mightier than a sword japo sisi tumebadili ukweli huu na kuuweka kinyume kiasi cha wageshi kuwa muhimu kuliko wahishimiwa.
            Nimalizie kwa kuhumiza usawa bila kujali tunayemjali ni mgeshi au mhishimiwa, msukuma mkokoteni au rubani au mtumwa na bwana na mtawaliwa na mfalme. Wote tulizaliwa uchi; na siku moja tutatoweka na kugeuka matope na kusahaulika. Tieni akilini;na kutenda haki mkijua kuwa ujivuni na ukatili havilipi; na malipo ni hapa hapa duniani. Pona haraka Tunduni Lissu. Aamina. Si utani. Hakika; natamani ungekuwa mgeshi au ndata kama si kuwa mwanachama wa chama twawala.
Chanzo: Nipashe J'mosi leo.

Wednesday, 4 October 2017

Is Magufuli’s presidency as bad as his critics claim?

Image result for photos of magufuli
There are calls and cries that President John Magufuli’s presidency is wanting. Those buying into such charges quote Magufuli, on different occasions, as saying that he wasn’t prepared to become president. This being the argument, let’s see if it is logical or just politicking.
I have a few reasons that rebut assertions that Magufuli is a president who is poised to nose-dive.
First, presidency is not a professional job; it is an institution that is not ran by an individual person namely the president. Presidency has many advisors that are specialised in many fields. Therefore, there is no way Magufuli can be treated as a wonky or wanting president.
Secondly, if you look at those making such allegations, some have their vendetta due to the fact that Magufuli’s regime has come up with a unique style of not budging when it comes to taking on the status quo. One of those who alleged that Magufuli is flabby to becoming president is former Prime Minister Fredrick Sumaye. We all know; Magufuli’s regime recently expropriated Sumaye’s farms. Such a person can’t see any good quality in Magufuli.
Thirdly, to know if Magufuli is fit or unfit for presidency, one must look at his track record as a minister; and thereafter as president. Apart from the father of the nation, Mwl Julius Nyerere, no president has ever attracted attention like Magufuli has recently. Refer to how many leaders the world over admire his brand of leadership. Indeed, nemo propheta in patria sua as the Latin sage has it that no one is considered a prophet in his or her homeland. Hate or love somebody. Again, give the devil his due. Looking at Tanzania today under Magufuli vis-à-vis fighting graft and managing public resources, I see a very shining star. Maybe, due to the fact that I’m not a politician, my lenses may be faulted.
Fourth, if one looks at how Magufuli is managing public funds and resources, he or she’ll be convinced that all noises about Magufuli’s unfitness for presidency become illogical and misguided so to speak. Methinks; the problem is the lack of the room for detractors for venting and politicking it was used under former regimes that used to underperform; and let tongues wag without necessarily reprimanding them. This is why many detractors are now eulogising such regimes while they hated them previously.
Fifth, to know if Magufuli fits the bill, look at service delivery in the country. Go to the hospitals, public offices and schools among others. People are now enjoying services they used to pine for previously. Pupils have desks to sit on; and, at least, some hospitals have beds for patients to sleep in. What’s wrong with such achievements?
Sixth, I couldn’t agree more with Magufuli when he says he isn’t a politician. Truly, he is not the type Tanzania was used to. He isn’t an artiste who tells lies in order to get away with murder. He says everything point black. For example, when he told the victims of famine that his government didn’t have food to dish out simply because it is unable; it was misconstrued as telling them to go to hell. Nay, did they want him to assure such victims that he’d solve the problem to end up not making good on it as they were used to?
Magufuli is not an angel. He is human. He therefore has some minor flaws to tweak i.e. denying political parties to do politics as they used to. So, too, Magufuli needs to listen to his advisors instead of courtiers and all those who want to take him for a ride by pretending they love and respect him while they actually are using him. One of those is one of his appointees accused of forging academic certificates. Such elements are dangerous to Magufuli’s presidency simply because they don’t tell him the truth. Instead, they dent his reputation in their attempts to please and thereby use him.
Another thing that Magufuli needs to tweak is his stance on the Draft Constitution. It is the right time for Tanzania to have a new constitution.  For, it is not only needed but also it’ll help him to take graft on.
In sum, those avowing that Magufuli isn’t fit for presidency are not doing him and Tanzania justice. They must wait and see how he’ll perform in the next elections after lapsing his five years in office. Keep it up Magufuli. Keep on as you rectify some shortfalls.
Source: Citizen Wed., today.

Shambulizi la Lissu tulete wapelelezi wa kigeni

            Sina shaka ninapoandika makala hii kusema kuwa jaribio la kutaka kumuua mbunge wa Singida Mashariki na rais wa Chama cha Wanasheria Tanzania (TLS) mheshimiwa Tundu Lissu ni suala lililochafua sifa ya Tanzania ukiachia mbali kuondoa imani kwa baadhi ya vyombo vya usalama. Hii ni kutokana na kushindwa lau kuwakamata wahusika pamoja na kujitahidi kufanya hivyo. Shambulizi hili la kishenzi na kikatili linakatisha tamaa kiusalama hasa ikizingitiwa kuwa si la kwanza. Na kwa hali ilivyo, huenda si la mwisho.
            Watanzania wanataka usalama na si usalama tu bali usalama wa uhakika. Watanzania wanakata wahalifu waliotaka kukatisha maisha ya Lissu wakamatwe, kujulikana na kuadhibiwa kwa mujibu wa sheria. Hata hivyo, hali ilivyo, uwezekano wa wahalifu hawa kukamatwa unazidi kufifia hasa ikizingatiwa kuwa muda unavyozidi kuyoyoma, ndivyo wahalifu wanavyozidi kuepuka kukamatwa. Wengi wanashangaa na kuhoji: je inakuwaje nchi yenye vyombo vyote vya usalama kushindwa na genge dogo la wahalifu? Je kweli tumeshindwa au tumeamua kushindwa?
             Asiyekubali kushindwa si mshindani. Nasi kama taifa tunalotaka kupambana na uovu na ukatili kama aliofanyiwa Lissu tukubali kushindwa. Tutakapofanya hivi –s kwa nia ya kuonyesha udhalili wala uhovyo bali kutaka kuwa na taifa salama –tutakuwa tayari kutafuta msaada kwa wenzetu. Hapa ndipo wazo la kutaka wapelelezi wa kigeni waitwe nao wajaribu. Hatutakuwa taifa la kwanza kufanya hivi. Alipouawa waziri wa mambo ya nje wa zamani wa Kenya Robert Ouko mwaka 1990, baada ya jeshi la polisi na vyombo vya usalama vya Kenya kushindwa kuwakamata waliomuua, vilimkodisha mpelelezi toka Uingereza aitwaye John Troon kuchunguza kadhia hii. Hata hivyo, Troon alipokaribia kuwagusa wasioguswa, alifungashiwa virago na kuondoka Kenya ili kuwanusuru wahalifu wakubwa waliokuwa wamejificha nyuma ya madaraka.  Sitaki nifananishe tukio la kushambuliwa Lissu na la kuuawa Ouko. Hata hivyo, tokana na kuwa mwanasiasa wa upinzani, wapo wanaojenga dhana kama hii kuwa woga unaweza kuwa kikwazo cha kuleta wapelelezi wa kigeni.
            Kwanini napendekeza tulete wapelelezi wa kigeni? Kwanza, hadi sasa hatujajua waliomshambulia Lissu, na kwanini walitaka afe. Pili, tokana na mkanganyiko na ukimya vilivyotawala, kuna uwezekano ikajengeka dhana ovu kuwa mamlaka yako nyuma ya shambulizi hili jambo ambalo kwangu haliingii akilini. Tatu, tokana na unyeti wa hadhi ya Lissu kama mpingaji mkubwa wa serikali, upo uwezekano maadui wa serikali–hasa walisiopenda mambo makubwa yanayofanywa na serikali kwa sasa kama kupambana na ufisadi na maovu mengine kiasi cha kuwatibulia waliozoea vya dezo–wanaweza kukodisha wauaji ili serikali ionekane imefanya hivyo. Nne, pia inawezekana wakawapo wabaya wake nchini wenye nafasi ambao wanaweza kutumia nafasi zao kuamuru Lissu auawe kwa kujipendekeza tu kwa mamlaka.  Hapa lazima tuondoe dhana kuwa shambulizi la Lissu linaweza kuwa uhalifu wa kaiwaida hasa tukizingatiwa namna, mahali na wakati liliopofanyika. Dodoma ni mji mkuu wa Tanzania. Eneo alipopigiwa risasi Lissu linaishi watu wazito wenye ulinzi wa uhakika. Na pia wahalifu hawa hawakuchukua chochote zaidi ya kutaka kuchukua uhai wa Lissu. Ukiunganisha haya yote, unaona ukubwa, unyeti na utata wa shambulizi hili la kigaidi na kiuaji.
            Tano, wahusika, yaani wanaopaswa kualika wapelelezi wa kigeni wanapaswa kujiuliza maswali machache muhimu. Je ingekuwa mimi, mwanangu, mke wangu, baba au mama yangu, rafiki yangu, mkubwa mwenzagu na mengine kama haya, ningetaka nifanyiwe nini wakati huu? Mbali na hili, wahusika wanapaswa kujua kuwa kama wataalika wachunguzi na wapelelezi wa kigeni, watakuwa wanakata kidomodomo cha wanaojenga dhana potofu kuwa kuna mkono wa serikali kwenye shambulizi dhidi ya Lissu tokana na polisi kushindwa kuwakamata wahusika. Pili, kwa kuleta wapelelezi wa kigeni, serikali itakuwa inazidi kuwajengea imani watanzania kuwa inajali sana usalama wao na amani ya taifa. Maana, shambulizi hili, licha ya kupunguza imani kwa serikali na vyombo vya usalama, imechafua amani na sifa vya taifa letu linalosifika barani kwa kuwa kisiwa cha amani ambacho sasa ni kisiwa cha amani kwa imani lakini si matendo. Kama wahalifu waliojaribu kumuua mtu mkubwa kama Lissu wanashindikana kupatikana, watakapoelekeza mitutu yao kwa walalahoi hali itakuwaje?
            Tumalizie kwa kuitaka serikali iliangalie shambulio la Lissu kwa mapana na kina zaidi ili kuepuka kupoteza sifa yake na ya taifa. Shambulio la Lissu si kwake tu bali kwa Tanzania hasa ikizingatiwa namna maadui zetu wanavyoweza kulitumia kutuchafulia jina kama ukimya na kutokamatwa kwa wahusika vitaendelea. Tutaonekana kama taifa lisilo imara tena; lisilo salama na lisilojali hata uhai wa watu wake jambo ambalo ni aibu na machukizo. Tusiwape maadui yetu la kusema kwa kudhani kuwa wauaji wa Lissu hawakamatwi kwa vile yeye ni mpinzani wa serikali. Hivyo, kuruhusu kujengeka dhana potofu kuwa serikali ilikuwa na mpango wa kumuondoa kwa vile anaonekana kuwa kikwazo. Tusifike huko. Mbali na hilo, tumuangalie Lissu kama mwanadamu yeyote mwenye haki ya kuishi hadi Mungu atakapotaka lakini si genge la magaidi uchwara.
Chanzo: Tanzania Daima J'tano leo.

Kijiwe kuwanyaka waliotaka kumdedisha Lissu

           Msomi Mkatatamaa anaingia akiwa na matabu makubwa mawili moja likiitwa How to Zap and Kill Uknown Killers na jingine, How To Make Uknown Known. Anayabwaga mezani akionyesha wazi kuwa na mawazo. Anaamkua na kuagiza kahawa yake. Mchunguliaji asiyepitwa na kitu ni wa kwanza kuchukua mojawapo na kuanza kusoma kana kwamba kimombo kinapanda.
            Kabla ya kumwaga sera, Kapende anamchokonoa “Msomi leo unataka kuturudisha chuo nini; mbona umekuja na ma-cyclopedia leo; kunani?”
            Kabla ya kuendelea Mgoshi Machungi anamkosoa “sema enseikoopidia siyo seikoopidia unatamka kama wasomi wa kisiku hizi wa chuo kikuu cha Manzese waliopata digii kwa vyupi.”
            Msomi anatikisa kichwa, kutabasamu na kuzoza “hujui kuwa sijakubali damu ya rafiki yangu Tunduni Lissu imwagike bure? Nipo najichua kitaaluma lau niweze kuwanyaka waliomfanyia kitu mbaya rafiki yangu halafu wakaachwa waendelee kutanua mitaani.” Anapiga chafya na kuendelea “nashindwa kuelewa ni kwanini geshi la polishi limeshindwa genge dogo la wapumbavu na wahuni kiasi hiki wakati lina ujuzi.”
            Kabla ya kuendelea Mipawa anajibu “sidhani kama limeshindwa. Kama limeshindwa basi limeshindwa kitu kimoja yaani kuwa na nia ya kuwasaka na kuwanyaka mbwa hawa wasio na huruma wala utu. Haiwezekani genge la majibwa wachache lituhangaishe kana kwamba hatuna wasomi wa security na intelligence. Kama limeshindwa, sasa linalipwa njuluku zetu kwa lipi wakati haliwezi kutuhakikishia usalama? Ni aibu ya mwaka kusema ukweli.”
            Kabla ya kuendelea, Mbwamwitu anamchomekea “japo mbinu zako ni za kisayansi na zinaingia akilini, angalia wasikunyotoe roho kama walivyotaka kumfanyia Tunduni mchana kweupe huku kamera zikinasa kila tukio lakini ndata wakashindwa kuwanyaka.”
            Mpemba anamchomekea Mbwamwitu “wallahi hawa hawamwezi Nsomi. Ninjuavyo mie japo hii siri, aweza uawa na SEAL peke yao wale waliomnyotoa roho bin Laden kule Aborabadi. Huyu tulie naye wengi hamnjui. Amewahi kutumiwa sana na FBI na M16 mbali na mashirika mengine ya kipelelezi duniani. Hata hivo, hii n siri. Huwa hataki julikana ingawa sie watu wake wa karibu tunjua hii kitu”
            Msomi anatabasamu na kuzoza “hapo nimekupata vilivyo. Kitaalamu, uhalifu uliotendwa na wanaojiita wasiojulikana ni simple. Mfano, nashauri tuunde timu yetu ya kijiwe kuwasaidia geshi kuona udogo wa suala linalowashinda. Lazima hawa mbwa wasiojulikana wajulikane kwa uba na uvumba.” Anakohoa na kuendelea “kama nilivyosema, ni rahisi kuwanyaka hawa mbwa kirahisi. Kwa ufupi, nitaonyesha ramani ya namna ya kuwanyaka. Kwanza, unaangiza CCTV camera zote za maeneo lilipotokea tukio uzione na kuzichunguza kujua nani walifika eneo husika. Pili, ukishindwa hili, unaweza kuitisha camera za barabarani ili kubaini ni magari mangapi yanayofanana na lile linalosemekana kuwabebwa magaidi uchwara hawa. Tatu, unamhoji Lissu na dereva wake kuona kama wanaweza kukupa lau picha ya watuhumiwa. Nne, unawahoji wahishimiwa wote waliowahi kulalamika na kuripoti kufuatiliwa na kundi hili uchwara. Na mwisho, unawanyaka wote unaowastukia kama vile yule mpumbavu aliyejitangaza wavuni kuwa alikuwa tayari kumdedisha Lissu kama angepewa ruhusa na anaowaabudia asijue ni ngurumbili wa kawaida watakaodedi siku moja.  Mwisho kabisa, baada ya kukusanya majina ya watuhumiwa na sura zao, nakwenda kwenye makampuni ya simu na kutaka mawasiliano yao mbali na kutaka yanipe simu zilizokuwa kwenye eneo hili mida lilipotokea tukio.  Maana, lazima makampuni ya simu yatakuwa na mawasiliano yao na locators za simu zilizokuwapo eneo husika. So simple. Hii ndiyo summary ya mkakati wangu wa kuwanasa wanaharamu hawa tena haraka. Natamani nimpige zongo huyu nguuwe waahi.”
            Baada ya kumaliza kuongea, kijiwe kinampigia makofi kwa kuonyesha umahiri katika masuala ya upelelezi aliyosomea kwa Joji Kichaka na kwa Maza huku mzee Maneno akichombeza “Ama! Kweli nyinyi ndiyo wasomi tunaowahitaji na siyo hawa wa kughushi kibashiteshite.”
            Kabla ya kuendelea Kanji anakula mic “mimi dugu yanguni iko tayari kuleta peleleji toka Bombei.” Hata kabla ya kumalizia sentensi yake, Mijjinga anamnyang’anya mic “Kanji acha utani. Unadhani gabacholi wanaweza kumpata mtu zaidi ya kumtoa njuluku na kulejea kwao kama walivyofanya akina Chavda na yule aliyetorosha twiga wetu na wengine wa RITES? Unadhani tumesahau siyo?”
            Sofia Lion aka Kanungaembe anamuunga mkono Mijjinga kwa kusema “hata mimi sikubaliani na Kanji hasa ikizingatiwa jamaa walivyo fisadi kinomi. Wao waendelee na mishemishe zao za kupiga njuluku zetu na kuwabagua ndugu zetu wanaofanya kazi jumbani yao.”
            Mgoshi Machungi anaamua kula mic “tena imetikumbusha yue mpumbavu aiyeomba ruusa amuue Tunduni. Je geshi iishamnyaka au naye anaeewe kama hawa wanaojiita wasiojuikana.”
            Mheshimiwa Bwege aliyekuwa akisikiliza kwa makini anaamua kutia guu “nadhani mmesema mengi. Kwanini tusiunde taskforce hapa hapa ili tukitoka hapa tuanze kazi ya kuwanasa hawa nguchiro. Chini ya uongozi wa SEAL Msomi sina wasi wasi tutawanyaka ndani ya siku mbili au tatu; au siyo?” akiwa anajiandaa si simu ya Msomi iliita! Kabla ya kujibu, anatuonyesha na kusema “unaona hii namba ya hatari? Ni ya rafiki yangu mkuu wa chuo cha kufundisha SEAL kule kwa Trumpet ananipa updates.
Chanzo: Tanzania Daima J'tano leo.

Monday, 2 October 2017

Huyu agombee unyekiti wa Chama Cha Mafisadi

Image result for photos of james rugemalira
Huyojamaa hapo juu akigombea unyekiti wa Chama Cha Mafisadi (CCM) wapiga kura wake waaminifu watakuwa wafuatao hapa chini na mitandao.Image result for photos of james rugemalira

Sunday, 1 October 2017

Magufuli ana uwezo wa kuwa kioo barani Afrika kama

Image result for photos of magufuli
Hakuna ubishi; rais John Pombe Magufulli sasa ni jina kubwa duniani. Hii ni kutokana na staili yake ya uongozi hasa kupambana na maouvu na kubana matumizi
Alipokataa kufanya ziara nje ya nchi wengi walisema mengi. Alinyamaza na kuendelea na mipango yake ya kuiweka Tanzania kwenye ramani ya dunia baada ya kupoteza umaarufu uliokuwa umejengwa na baba wa taifa Mwl Julius Nyerere. Kwa msimamo na staili ya Magufuli, uwezekano wa kuwa kioo na si kiongozi tu wa Tanzania bali Afrika ni mkubwa. Hata hivyo, kuna mambo machache anayopaswa kufanya Magufuli ili kuweza kufikia hadhi hii adhimu duniani.
Leo nitadurusu baadhi ya mambo yanayoonekana kumharibia au kukwamisha, kama si kupunguza, sifa za rais Magufuli.
Mosi, kama atataka kuwa kioo mithili ya wachache kama vile Nelson Mandela, rais wa kwanza mweusi wa Afrika Kusini na kwa mbali marehemu Ketumire Masire wa Botswana, anapaswa kuachana na kuvizuia vyama vya upinzani kumpinga na kufanya siasa. Kwani, hakuna jambo linalomtia doa Magufuli kama katazo hili linalofanya baadhi ya wakosoaji wamshuku uimla jambo ambalo bado si kweli.
Pili, Magufuli ameonyesha nia na ujasiri mkubwa katika kupambana na ufisadi nchini chini ya dhana yake ya kutumbua majipu. Mfano wa karibu ni pale alipochaguliwa kuwa mwenyekiti wa Jumuia ya Afrika Mashariki. Kwa ushupavu wa hali ya juu, alipunguza na kubana matumizi. Hata hivyo, katika azma yake ya kupambana na ufisadi, Magufuli ameonyesha kupwaya pale alipokumbana na watu wake wa karibu kama vile Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda anayetuhumiwa kughushi vyeti vya kitaaluma. Ni bahati mbaya kuwa si Magufuli wala Makonda aliye tayari kupambana na kadhia hii vilivyo kwa kuzingatia kanuni za uwajibikaji na utendaji haki. Ingawa Magufuli, na hata Makonda, wanaweza kudhani hili limepita, halijapita. Watanzania na ulimwengu bado wanahitaji maelezo na majibu yanayoingia akilini kuhusiana na ukweli wa mambo. Kimsingi, Makonda, kati ya watu walioutia doa utawala wa Magufuli, anaweza kuchukua namba moja.
Japo Magufuli amejitahidi kuwa kimya, ukiachia mbali kusema wazi kuwa hatamuondoa Makonda, kuna madhara makubwa atakayopata. Kwani, kadhia hii inamuonyesha kama mtu mwenye upendeleo, kulindana na kujuana. Mbali na Makonda, ni ile kauli ya Magufuli kuwa hatawachunguza watangulizi wake wanaoshutumiwa kwa ufisadi katika tawala zao. Magufuli alisema kuwa tuwaache wazee yaani watangulizi wake wastaafu vizuri wakati kuna kelele kuhusiana na namna tawala zao zilizyoingiza nchi kwenye dimbwi kubwa la ufisadi kama vile kutunisha deni la taifa bila maelezo, kuingia mikataba mibovu ya uwekezaji inayomhangaisha Magufuli kwa sasa ukiachia mbali matumizi mabaya ya madaraka, fedha na raslimali za taifa. Kwa wanaojua namna haya mambo yalivyofanyika, Magufuli hawezi kuisafisha Tanzania bila kufanya yafuatayo:
Mosi, kuacha sheri ifuate mkondo wake bila kujali cheo wala ukaribu wa mhusika. Pia haiwezekani Magufuli akaonekana anatenda haki ilhali kuna wasioguswa kwenye utawala wake. Mfano wa karibu ni ile hali ya zoezi la kubaini na kushughulikia walioghushi. Kuna wanaoamini kuwa zoezi hili liliuawa baada ya Makonda kujikuta hana utetezi kuhusiana na kashfa zinazomkabili.
Tatu, Magufuli amekuwa akisikiliza upande mmoja wa wanaomuunga mkono hata kutaka kumtumia kwa kujifanya wanapenda huku wakimmwagia sifa lukuki ili kulinda kitumbua chao. Kimsingi, kama kiongozi wa taifa, Magufuli anapaswa kusikiliza wote bila kujali itikadi zao. Anachopaswa kuzingatia ni mantiki na mashiko ya hoja wanazotoa wakosoaji. Yeye ni binadamu; na si Mungu. Na isitoshe yupo madarakani kuwatumikia watanzania wote kwa usawa bila upendeleo wala uonevu. Mfano mzuri ni ule wa marehemu baba wa taifa Mwl Nyerere aliyewahi kuacha watu wake wa karibu kama vile marehemu Chadiel Mgonja alipokabiliwa na tuhuma za uoza mbali na marehemu Abdallah Fundikira alipokabiliwa na tuhuma za kula rushwa. Aliwaacha wakabeba mizigo yao au kuwawajibisha bila kujali uchapakazi wao wala ukaribu wao kwake. Huu ndiyo uongozi wa mfano; na ndiyo maana Mwl Nyerere ameendelea kuwa maarufu hata baada ya kufariki. Huu ni mfano na msaada wa hali ya juu kwa rais Magufuli kama ataamua kuufuata.
Mbali na mapungufu hayo hapo juu, Magufuli amejitofautisha na watawala wengi wa kiafrika wanaopenda kutumia ofisi za umma kwa manufaa binafsi wakifuja mali na ofisi za umma bila kujali kuwa wanaongoza watu maskini. Mfano, Magufuli hajawahi kuhudhuria mikutano mingi ya kimataifa ambayo, mara nyingi, ni mzigo kwa taifa. Rejea alivyoacha kuhudhuria kikao cha 72 cha wakuu wa Umoja wa Mataifa kinachoendelea ambapo viongozi wengi hukutana na kuishi kwenhye mahoteli ya bei mbaya huku walipa kodi wao maskini wakitwishwa zigo hili. Kwa hili, tunampongeza na kumuomba aendelee hivyo bila kujali kelele za wanaomtuhumu kwa kutoiwakilisha Tanzania kwenye vikao hasara vya kimataifa.
Tumalizie kwa kumshauri rais Magufuli aweke sawa, pamoja na mengine, mambo tuliyoainisha hapo juu. Mungu ibariki Tanzania. Mungu mbariki rais Magufuli.
Chanzo: Tanzania Daima J'pili leo.